Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.

Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.a.w.) alishikwa na ugonjwa wa kuumwa kichwa na homa. Lakini muda wote alikuwa akijitokeza kufanya shughuli zake kama kawaida. Katika hali hiyo hiyo ya kuumwa, alikwenda Uhud na kuwaombea dua mashahidi waliozikwa mle. Pale alitoa khutuba ifuatayo:



“Siwahofii kuwa mtajihusisha na kuabudu masanamu baada yangu, lakini nahofia kuwa mtajihusisha sana na dunia kiasi cha kufikia hatua ya kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kisha, mkishafanya hivyo, mtaishia kwenye maangamivu kama walivyoangamia wa kabla yenu”.



Mtume(s.a.w.) pamoja na maradhi yake aliendelea kuswalisha swala za jamaa msikiitni na bado alikuwa akitimiza ngono za wake zake wote tisa. Ugonjwa ulipozidi kushitadi, aliwaomba wakeze kuwa waje kumuuguza kwa Bibi Aysha(r.a.) palipo kuwa karibu na msikiti. Wakeze walikubali kwa moyo mkunjufu. Ugonjwa ulivyoendelea Mtume(s.a.w.) alizidi kuwa dhaifu na hatimaye alishindwa hata kuhudhuria swala za jamaa msikitini. Aliposhindwa kuhudhuria msikitini alitoa amri Abubakar awe anaongoza swala ya jamaa, alifanya hivyo kwa siku kadhaa.



Siku nne kabla ya kufariki kwake, Mtume(s.a.w.) alijisikia nafuu kidogo na akakoga kabla ya swala ya Dhuhuri. Baadaye alikuja msikitini akiwa amesaidiwa na watu wawili, Abbas(r.a.) na Ally(r.a.). Abubakar alikuwa anaendelea kuongoza swala kama kawaida. Alipomuona Mtume(s.a.w.) anakuja alianza kuondoka, lakini Mtume alimuambia abakie pale pale naye akakaa pembeni mwake. Baada ya swala alihutubia kama ifuatavyo:



“Allah amempa mja wake achague kati ya dunia na akhera. Akachagua akhera. Ninawausia, Enyi Waislamu (Muhajirina) muwe wema kwa Ansar. Hakika wametekeleza wajibu wao vizuri. Waislamu kwa ujumla wao idadi yao itaongezeka lakini Ansar watapungua na kuwa kama chumvi katika chakula. Zimeangamia umma zilizotangulia ambazo ziliabudu makaburi ya Mitume wao na ya watu wema. Ninawakatazeni kufanya hivyo. Nina deni kubwa (la Ihsani) kwa Abubakar. Kama ingekuwa nimfanye yeyote kuwa rafiki yangu, angalikuwa Abubakar, lakini uhusiano (udugu) wa Uislamu unatosha. Ee, binti yangu Fatimah na Ee, shangazi yangu mpendwa, Swafiyah, fanyeni amali kwa ajili ya akhera kwani sitaweza kuwasaidia chochote dhidi ya hukumu ya Allah.23



Hii ilikuwa khutuba ya mwisho ya Mtume (s.a.w.). Kisha ugonjwa ulishitadi. Alijisikia nafuu kidogo asubuhi ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul-Awwal, 11 A.H, lakini ilipofika adhuhuri hali ilibadilika tena kuwa mbaya. Alikuwa akizimia kila baada ya muda mfupi. Hata alipokuwa katika hali hii ya sakaratul-maut, bado hakumsahau Mola wake. Muda wote alikuwa akisema “Nisamehe Bwana wangu”. Wakati wa alasiri alipokuwa anapumua pumzi za mwisho mwisho, alisikika kwa sauti ndogo akisema:

“Shikamana na swala na wafanyieni wema watumwa (wafungwa)”.



Palikuwa na beseni la maji lililowekwa karibu na Mtume (s.a.w.). Alikuwa akilowesha viganja vyake mara kwa mara kwenye maji haya na kufuta uso wake, huku akisema, “Enyi watu! Hakika kutoka roho kuna machungu makubwa”. Wakati huo aliingia mtu mmoja na mswaki mkononi mwake. Mtume akaashiria apewe mswaki huo. Alitafuniwa na Bibi Aysha, ambaye alimpakata mapajani mwake, na kumpa akawa anaswakia kidogo kidogo. Kisha akiwa ameashiria kwa kidole (cha shahada) na huku ametazama juu alisema mara tatu:



“Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,

Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,

Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu”.



Roho yake ilirudi kwa Bwana na Mola wake mtukufu wakati wa jioni ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul Awwal, 11 A.H, Sawa na tarehe 8 Juni 632 A.D. Mtume(s.a.w.) alifariki akiwa na umri wa miaka 63. Mazishi yake yalifanyika siku iliyofuatia. Waliomwosha ni jamaa zake wa karibu – Fadhil bin Abbas, Ally bin Abu Talib na Usamah bin Zaid(r.a.). Kisha alizikwa kwenye chumba cha Bibi Aysha(r.a.) pale pale alipofia. Hivi sasa kaburi la Mtume(s.a.w.) limo ndani ya Msikiti wa Madinah.




“Ee Allah! Mrehemu Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki “Ee Allah! mbariki Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Download App yetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2193

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Maadui wakubwa wa dola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.

Soma Zaidi...
Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri

Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a.

Soma Zaidi...
HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

Soma Zaidi...
fadhila za kusoma quran

Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1.

Soma Zaidi...
Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)

Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.

Soma Zaidi...
tarekh 5

KUZALIWA KWA MTUME (S.

Soma Zaidi...