a) Wajibu wa Khalifa kama kiongozi wa Dola
i. Kujenga maisha ya binaadamu katika misingi ya Ucha – Mungu na matendo mema.
Rejea Qur’an (57:25)
ii. Kutumia uchumi wa Dola katika kukuza na kuendeleza maadili ya raia wake.
iii. Kuamrisha mema na kukataza mabaya katika jamii kupitia njia zifuatazo;
- Kuteua Makadhi wacha – Mungu na waadilifu kwa kusimamia sheria.
- Kuteua Madai’yah (walimu) wa kufundisha mambo muhimu ya dini na maisha kwa ujumla.
- Khutba za Ijumaa na Sikukuu za Eid zilitumika kuelimisha waumini.
- Kuteua tume (jopo) la watu kwa ajili ya kufuatilia tabia na mienendo ya watu na kutoa adhabu.
iv. Kulinda mipaka ya Dola kwa gharama yeyote, kwa vita au diplomasia.
v. Kuteua viongozi wa ngazi mbali mbali kwa kushirikiana na Shura yake ya watu maalum.
vi. Khalifa ndiye mkuu wa majeshi na ndiye amir – jeshi anayeamua vita ipiganwe au isipiganwe kwa kushirikiana na watu wa shura.
vii. Khalifa pia ndiye mwanasheria mkuu wa Dola ya Kiislamu, anayesikiliza kesi na kutoa hukumu.
b) Mgawanyo wa viongozi wengine waandamizi wa Dola na Majukumu
- Vyombo vikuu vya utendaji katika kuendesha Dola ni pamoja na;
1. Kamati kuu ya utendaji
2. Shura ya waumini (watu) wote
3. Tume ya kufuatilia malalamiko ya raia.
- Dola iligawanywa katika majimbo na wilaya na kuwa na viongozi wafuatao;
1 Walii – Gavana,
2 Amil – mkusanyaji wa mapato ya Dola
3 Kadhi – jaji kwa ajili ya kusimamia sheria na kutoa hukumu.
c) Vyanzo vya Mapato na Uchumi wa Dola ya Kiislamu
Zifuatazo ni miongoni mwa vyanzo vya uchumi wa Dola ya Kiislamu:
i. Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali
(Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.
ii. Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.
iii. Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.
iv. Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya
Kiislamu Madinah.
v. Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.
vi. Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.
vii. Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.
d) Ulinzi na usalama wa Dola ya Kiislamu wakati wa Makhalifa
- Wakati wa Ukhalifa ulinzi na usalama uliimarishwa kwa kiwango kikubwa.
- Kinyume na wakati wa Mtume (s.a.w) hapakuwa na jeshi maalum la ulinzi na usalama wa Dola, bali kila muislamu mwanamume alikuwa askari.
- Wakati wa Makhalifa pamoja na kila muislamu kuwa askari lakini kulikuwa na jeshi maalum kwa ajili ya ulinzi wa Dola na raia.
- Kulikuwa na askari wa farasi, wa miguu na la wanamaji lililoanza wakati wa
Ukhalifa wa Uthman (r.a).
- Kuliimarishwa zaidi kwa Idara ya ulinzi na usalama ukilinganisha na wakati wa Mtume (s.a.w).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 663
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?
Mwenyezi Mungu si kiumbe. Soma Zaidi...
Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...
HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...
Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s) na kumkabili (kumlingania) firauni
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...
HARAKATI ZA DINI WAKATI WA MATABIINA NA TABII TABIINA
Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...
Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa
Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a. Soma Zaidi...
Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...
Nabii Isa(a.s) Alitumwa kwa Wana wa Israil
Mtume Isa(a. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa Tawala za kifalme baada ya uongozi wa Makhalifa.
Kuanzishwa Ufalme. Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...