UPUNGUFU WA VITAMINI C



Endapo kutatokea upungufu wa vitamini C mwilini kuna athari kubwa itakayotokea mwilini ikiwemo:
1.Kupata ugonjwa wa kiseyeye
2.Kuchelewa kupona kwa vidonda
3.Kutokwa na damu kwenye mafinzi
4.Maumivu ya mifupa
5.Maumivu ya misuli na viungio


ATHARI ZA KULA VITAMINI C KUPITILIZA
Kila kirutibisho kinahitajika ndani ya miili yetu kwa kiwango maalumu. Endapo kirutubisho kitakuwa kingi kupitiliza athari zinaweza kutokea katika afya ya mtu. Miongoni mwa athari za kuwa na vitamini C kupitiliza ni kama zifuatazo:-


1. Kichefuchefu
2.Maumivu ya tumbo
3.Kuharisha
4.Kufanyika kwa vijiwe ndani ya figo
5.Kujaa kwa tumbo


Mwisho
Kwakuwa sasa unatambua umuhimu wa vitamini C ndani ya mwili wako. Hakikisha kula vyakula vyema ili kusaidia katika kuboresha afya yako. Endelea kuwa pamoja na si kwa makala nyingine za Afya.