Nini maana ya protini

Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa

Nini maana ya protini


NINI MAANA YA PROTINI


Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.


Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)


Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes


Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1244

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Faida za kiafya za kula nyama

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama

Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin E

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin E

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula spinach

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach

Soma Zaidi...
Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Faida za kula Palachichi

Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako

Soma Zaidi...
Vyakula vya protini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya protini

Soma Zaidi...
Karoti

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karoti

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu maji, kazizake mwilini na athari za upungufu wake mwilini

Hpa utafahamu faida za maji mwilini pamoja na athari za upungufu wa maji mwilini na dalili zake

Soma Zaidi...