Figo ni nini, ni yapi maradhi yake na nitajiepusha vipi na maradhi ya figo

Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.

Figo ni nini, ni yapi maradhi yake na nitajiepusha vipi na maradhi ya figo

IJUWE FIGO NA MARADHI YAKE NA NAMNA YA KUJIKINGA NA MARADHI YA FIGO:

Figo ni katika viungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ijapokuwa kila kiungo ni muhimu kwenye mwili wa binadamu, lakini katika mfumo wa kutoa mkojo na kuchuja damu figo ni muhimu zaidi. maradhi ya figo yamekuwa yakiongezeka kuliko ilivyokuwa hapo zmani, ijapokuwa kasi yake sio sawa na maradhi mengine. Makala hii itakwenda kukueleza ni nini hasa hizi figo, na ni yapi maradhi yake na ni kwa namna ggani utaweza kujilinda na maradhi ya figo.


Kila mtu ana figo mbili kwenye mwili wake, ukubwa wa figo unakadiriwa kufukia ukubwa wa ngumi yako. Katika mwili wako figo hupatikana karibia na katikati ya mgongo chini kidogo ya mbavu. Ndani ya kila figo kuna mamilioni ya vichujio vya kuchuja damu vinavyojulikana kama nephron. Kazi yake kubwa ni kuchuja damu, kuondoa uchafu kwenye damu na kuondoa maji ya ziada kwenye damu na kupata mkojo ambao ni mchanganyiko wa majina na uchafu uliotoka kwenye damu. Baadaye maji haya ya mchanganyko yanakwenda kwenye kibofu na kuhifadhiwa kama mkojo.



Kati ya maradhi mengi ya figo huanza kuathiri hizi nephone. Na endapo hizi nephrone zikiharibiwa zinapelekea figo kuathirika na kushindwa kufanya kazi vyema na kushindwa kuondoa uchau kwenye damu. Katika sababu za tatizo hili la kuathirika kwa nephone inaweza kuwa matatizo ya kurithi, majeraha, ama matumizi ya madawa ambayo athari yake yanaweza kuathiri figo.



Unaweza kuwa hatarini sana kama una maradhi ya kisukari, ama kama una shinikizo kubwa la damu ama una ukaribu wa kifamilia na watu ambao wana tatizo hili. Maradhi hatari ya figo ni yale ambayo huathiri nephone kipolepole na huwenda hii kuchukuwa miaka kadhaa hadi kuja kuumwa. Matatizo mengine yanayoweza kuathiri figo ni kama saratani ya figo na vijiwe vya kwenye figo.



Katika njia za kulinda figo yako dhidi ya maradhi ni pamoja na kunywa maji mengi angalau glasi 8 kwa siku. Fanya mazoezi na punguza kula vyakula vyenye chumvi sana. Nenda chooni kila unapohisi kukojoa wacha kubana mkojo kwa muda mrefu. Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zitakusaidia kulinda figo zako dhini ya maradhi.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 935

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Dalili za ugonjwa wa Ugumu wa kumeza (dysphagia)

Ugumu wa kumeza (dysphagia) inamaanisha inachukua muda na bidii zaidi kuhamisha chakula kutoka kwa mdomo wako hadi kwenye tumbo lako. Ugumu wa kumeza unaweza pia kuhusishwa na maumivu. Katika baadhi ya matukio, kumeza inaweza kuwa haiwezekani. Ugumu w

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa UTI

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI

Soma Zaidi...
AFYA NA MAGONJWA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
NI WATU GANI WALIO HATARINI ZAIDI KUPATA UKIMWI?

Post hii itakwena kukufundisha kuhusu historia fupi ya Ukimwi na matibabu yake. Ni wapi wapo hatarini kupata maambukizi na ni kitu gani wafanye?

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu ugonjwa wa vidonda vya tumbo (Peptic ulcers)

Vidonda vya tumbo ni vidonda vilivyo wazi vinavyotokea kwenye utando wa ndani wa umio, tumbo na sehemu ya juu ya utumbo wako. Dalili ya kawaida ya Peptic ulcer ni maumivu ya tumbo. Vidonda vya tumbo ni pamoja na: Vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani

Soma Zaidi...
Dalili za uvimbe kwenye kinywa

Post hii inahusu dalili za uvimbe kwenye kinywa ambapo kitaalamu hujulikana Kama oral candidiasis Uvimbe kwenye kinywa husababisha vidonda vyeupe, kwa kawaida kwenye ulimi au mashavu ya ndani. Wakati mwingine uvimbe kwenye kinywa huweza ku

Soma Zaidi...
dondoo 100

Basi tambua haya;- 1.

Soma Zaidi...
HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO

HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupunguza hatari yako ya vidonda vya tumbo ikiwa unafuata mikakati sawa inayopendekezwa kama tiba ya nyumbani kutibu vidonda.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kushoto

Soma Zaidi...