Dalili za ukimwi siku za mwanzo

Makala hii inakwenda kukupa majibu ya maswali mengi kuhusu VVU na UKIMWI. tutakwenda kuona kwa ufupi historian a chanzo cha VVU na UKIMWI. hatuwa za maambukizi ya VVU na ukimwi na dalili zake za kuonekana toka kupata maambukizi. Pia hapa utajifunza namna

Dalili za ukimwi siku za mwanzo

DALILI ZA UKIMWI SIKU ZA MWANZO
Bila shaka umeshawahi kujiuliza kuhusu dalili za mwanzo za VVU na ukimwi. Makala hii itakwenda kujibu baadhi ya maswali yako mengine ambayo ulikuwa ukijiuliza kama, ni zipi dalili za mwanzo za vvu na ukimwi, je ukimwi unaingiaje, ni nini kitatokea baada ya kupata virusi vya ukimwi na mengineyo zaidi. Makala hii ni moja ya makala zetu za kutoa elimu ya afya ili kuendelea kuelimusha jamii.



Je nini maana ya UKIMWI?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno Upungufu Wa Kinga Mwilini. Ukimw husababishwa na aina ya virusi inayojulikana kwa jina la VVU yaani Virusi vya ukimwi. Historia ya Ukimwi imeanza zamani sana toka miakaya 1950. Kuna nadharia nyingi sana kuhusu chanzo na asili ya ukimwi. Kisayansi nadharia inayokubalika ni kuwa chanzo cha ukimwi ni masokwe. Miaka ya 1980 ukimwi ndipo ulipoanza kujulikana rasmi.


Hatua za maambukizi ya VVU na UKIMWI
Mara tu baada ya mtu kupata maambukizi mapya, atapitia hatuwa kuu tatu kabla ya kuambiwa ana ukimwi. hatuwa hizi hutofautiana kwa dalili zake. Kutoka kuambukizwa virusi mpaka kuambiwa mtu ana ukimwi inaweza kuchukuwa miaka mitano hadi kumi. Wapo baadhi ya watu wakawa pungufu ya hapo ama Zaidi ya hapo. Hebu saa tuzione hatuwa hizi na dalili zake.



A. Hatuwa ya kwanza baada ya maambukizi mapya:
Hatuwa hii hupatikana mwanzoni mwa wiki za mwanzo kabisa baada tu ya kupata maambukizi mapya. Katika hatuwa hii mtu hawzi kupima akaonekana kuwa ana maambukizi. Katika hatuwa hii virusi vinakuwa ni vingi sana kwenye damu, na huzaliana kwa kasi sana. Na hapa mtu anaweza kuonyesha baadhi ya dalili. Kuonyesha dalili hizi inachukuwa wiki 2 hadi sita. Baada ya hapo hatoweza kuona dalili tena. Dalili za maambukizi ya VVU katika hatuwa hii ni kama:-

1. Kupata mafuwa
2. Vidonda vya koo
3. Uchovu
4. Homa
5. Maumivu ya kichwa
6. Kutokwana upele
7. Kuvimba na kuuma kwa tezi za shingo na mapajani.



B. Hatuwa ya pili baada ya baambukizi mapya
Hatuwa hii ni katika hatuwa hatari sana. Katika kipindi hiki kiwango cha virusi kwenye damu hupunguwa na virusi kuelekea maeneo mengine ya mwili na kuathiri seli hai nyeupe zinazojulikana kama VD4. Katika hatuwa hii mtu akipima ataonekana kama ameathirika, lakini hakuna dalili yeyote itakayoonekana kwa muathirika katika kipindi hiki chote. Hatuwa hii inaweza kudumu kwa muda wa miaka mitano hadi 10. Katika wakati huu wote virusi vitaendelea kuathiri na kuharibu seli za CD4 mabzo ndio mlinzi wa mwili.


Seli za CD4 ni nini na ni zipi kazi zake?
Kabla hatujaona hatuwa ya tatu kwanza tuone kwa ufupi ni nini seli za CD4. Katika damu kuna seli aina kuu tatu ambazo ni seli hai nyeupe, seli hai nyekundu na seli sahani. Kila moja kati ya hizi ina kazi yake maalumu. Kwa mfano:-



1. Kazi za seli hai nyekundu ni kusafirisha hewaa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu na kupeleka kwenye moyo ambapo husambazwa kuelekea maeneo mengine ya mwili. Seli hai nyekundu ndizo ambazo nyingi kwenye damu na ndio maana damu ni nyekundu. Pia kazi nyingine ni kusafirisha hewa ya kabonidaiyoksaidi kutoka kwenye seli kupeleka kwenye mapafu kupitia kweye moyo.



2. Kazi za seli sahani ni kusaidia katika kuganda kwa damu na kupona kwa vidonda. Endapo utakuwa umejikata na jeraha likawa linatoa damu, seli sahani hiletwa kwa wing eneolile ili kusaidia damu kutoendelea kutoka na kuganda eneo lile. Uponaji wa vidonda na majeraha pia huhitaji seli hizi.


3. Seli hai nyeupe kazi zake ni kulinda mwili zidi ya vijidudu vya maradhi kama bakteria, fangasi, virusi na protozoa. Kwa ufupi seli hizi ni kama ndio walinzi wa mwili endapo zitapunguwa mwili utakuwa hatarini. Seli hizi hutafuta vijidudu hivi popote vilipo na kuviuwa kwa kuvimwagia kemikalia mbazo zitavifanya vife. Seli hai yeupe ndizo huitwa cd4. Kwa hiyo kazi kuu ya seli za CD4 ni kupambana na vijidudu shambulizi ndaniya mwili.



Sasa virusi vya ukimwi (VVU) vinapoingia mwilini moja kwa moja hutafuta seli za CD4, Huziingia ndani yake na kuanza kuzaliana humo. Baada ya kuwa virusi bni vingi ndani ya sli hiyo hupasuka na kumwaga virusi nje, na seli ile hufa kabia. Maelfu ya virusi hivi vilivyitoka kwenye seli moja huvamia seli nyingine na mhakato hujirudia. Baada ya muda wa miaka kadhaa mtu huyu atakuwa na upungufu wa kinga mwilini na hapo ndipo huambiwa ana ukimwi.



C. Hatuwa ya tatu (ukimwi).
Kikawaida mtu mwenye afya aha seli za cd4 500 mpaka 1500 kwenye kipimo kimoja. Sasa kama ana VVU huanza kuharibu seli hizi hadi hupunguwa chini ya kiwango hiko. Zikipunguwa kutoka 500 hadi 200 hapa huambiwa mtu huy ana upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. tafiti zinaonyesha kuwa baada ya kufikia hatuwa hii ya cd4 200 kama mtu huyu hataanza matibabu maalumu itachukuwa mikaa mitatu hadi kufariki. Hatuwa hii mgonjwa ataanza kuona dalili za ukimwi ambazo ni:-

1. Kupunguwa uzito kwa asilimia 10 bila ya sababu maalumu
2. Kuharisha mfululizo
3. Kuota upele kuzungukia maeneo mbalimbali ya mwili hadi sehemu za siri
4. Kuota majipu
5. Kusumbuliwa na fangasi mara kwa mara
6. Kuwa na homa za mara kwa mara
7. Kukonda sana bila ya sababu maalumu
8. Kuwa na uchovu wa mara kwa mara
9. Kupata maradhi nyemelezi kama kifua kikuu, kisukari, saratani, mkanda wa jeshi na mengineyo.



Nini mtu afanye baada ya kugundulika kuwa ni muathirika?
Vyema kwanza kupata ushauri kutoka kwa mtoa huduma ya ushauri nasaha. Hii itasaidia kumuweza mtu vyema kiakili, na kumuandaa kukabiliana na changamoto. Pia itamsaidia kujifunza Zaidi kuhusu namna ya kuishi na virusi vya ukimwi. pia atatakiwa kuanza matibabu haraka iwezekanavyo. Matibabu haya yatamsaidia ku:-

1. Kupunguza uzalishaji wa virusi vipya ndani ya mwili
2. Kuzuia virusi vya ukimwi visiharibu seli nyingine za mwili
3. Kumfanya mtu asifike kwenye hatuwa ya tatu ya kuambiwa ana ukimwi
4. Kupunguza uwezo wa mtu kumuambukiza mwingine.



Ni muda gani virusi huonekana kwenye kipimo?
Vipimo vya VVU vipo katika makundi kadhaa. Vipo ambavyo hipima kwa kutumia damu, vipo kwa kutumia mate. Tukiacha mbali hayo yote ni kuwa virusi vya ukimwi huanza kuonekana baada ya wiki tatu jhadi miezi mitatu kwa ajili ya uthibitisho Zaidi. Pia vipo vipimo ambavyo kuweza kuonyesha mapema Zaidi ila mara nyingi hivi havipatikani kwa urahiri.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 667

Post zifazofanana:-

Nikiwa katika siku zangu siumwi ila tatizo Ni kwamba najisikia kichefu chefu
Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Haki na wajibu wa mke kwa mumewe na familia
Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu maumivu ya jino
Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino Soma Zaidi...

English tenses test 006
Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
Soma Zaidi...

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...

Haya ndio yanayobatilisha Hija
Soma Zaidi...

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU
Soma Zaidi...

HADITHI YA KHALID MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID. Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...