Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.

Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.

Post hii inahusu zaidi Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hali hii uwatokea sana wanawake zaidi ya wanaume, kwa kitaalamu hali hii ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo huitwa cystitis.

Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.

1. Uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo usababishwa na bakteria ambao uingia na kushambulia sehemu za ndani za kibofu Cha mkojo, bakteria hao wanaweza kutoka sehemu mbalimbali kama vile kwenye mkojo wenyewe ikiwa mkojo umekaa kwa mda mrefu bila kutolewa nje hao bakteria wanaweza kushambulia sehemu za ndani ya kibofu Cha mkojo na hatimaye kuleta maambukizi kwenye kibofu Cha yanayoambatana na uvimbe.kwa hiyo ni lazima kukojoa tu baada ya kuhisi mkojo Ili kuepuka madhara ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.

 

2. Kutumia sana ngono zembe yaani kujamiiana bila kutumia kondomu.

Hii ni mojawapo ya sababu ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa ya ngono ambapo bakteria kutoka kwa mtu Mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine ambaye Hana maambukizi na kusababisha kuwepo kwa bakteria ambao uingia kwenye kibofu Cha mkojo na kushambulia na kusababisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hasa hasa kama bakteria hawa wasipotibiwa  mapema uweza kuleta madhara makubwa zaidi na kusababisha ugumba. Kwa hiyo tunapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana.

 

3. Kuaribika kwa sehemu za kuchuja mkojo.

Wakati mwingine Kuna kuharibika kwa sehemu mbalimbali zinazohusika na kuchuja mkojo, kama vile figo, nephroni na sehemu zote kwa hiyo hali hii usababisha bakteria kusababisha maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu mkojo hauwezi kutoka kwa wakati au pengine kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo, hali ambayo usababisha bakteria kuendelea kusababisha maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo. Kwa hiyo tunapaswa kuangalia mfumo wote wa kibofu Cha mkojo.

 

4. Kutumia catheter kwa mda mrefu au mara kwa mara.

Hii ni sababu mojawapo ambayo ufanya kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, kwa sababu catheter inaweza kuharibu kwenye milija wa mkojo na kusababisha bakteria kuingia na kuleta madhara makubwa ambayo yanasababisha kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa hiyo inabidi catheter kuwepo kwa mda unaohitajika, mda isizidi Ili kuzuia maambukizi.kwa hiyo wataalamu wa afya wanapaswa kuhakikisha kuwa catheter unatolewa kwa mda.

 

5. Wanawake wanaotumia uzazi wa mpango.

Wanawake wengi wanaoweka mipira kwaenye uke illi kuzuia  mimba isitungwe usababisha bakteria kupita na kuingia kwenye sehemu ya kibofu Cha mkojo na kuleta madhara makubwa zaidi ambayo yanaweza kusababisha uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu mipira hiyo uacha uwazi ambao usababisha bakteria kuweza kupita na kuzaliana huko na kuleta uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 3791

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 ai web app     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Athari za kutotibu fangasi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za kutokutibu fangasi

Soma Zaidi...
Jinsi ya Kupunguza Mafuta ya Tumbo

Kupunguza mafuta ya tumbo si tu suala la muonekano, bali ni hatua muhimu kwa afya njema ya muda mrefu. Posti hii inaangazia mbinu za kisayansi zinazohusisha lishe bora, mazoezi madhubuti, na mabadiliko ya mtindo wa maisha ili kukusaidia kupunguza uzito kwenye eneo la tumbo kwa ufanisi.

Soma Zaidi...
VIRUSI VYA KORONA AU CORONA (CORONAVIRUS)

Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu.

Soma Zaidi...
Athari za ugonjwa wa Homa ya inni

Posti hii inahusu zaidi adhari za ugonjwa wa Homa ya inni, hizi ni athari ambazo zinaweza kutokea ikiwa ugonjwa huu wa inni haujatibiwa, zifuatazo ni athari za ugonjwa wa inni

Soma Zaidi...
Namna magonjwa ya koo yanavyosambaa

Posti hii inahusu zaidi namna ya magonjwa ya koo yanavyosambaa, magonjwa haya usambaa kutoka sehemu Moja kwenda nyingine kwa njia tofauti kama ifuayavyo

Soma Zaidi...
Dalilili za mimba Kuharibika

Kuharibika kwa mimba ni upotevu wa hiari wa ujauzito kabla ya wiki ya 20. Takriban asilimia 10 hadi 20 ya mimba zinazojulikana huisha kwa kuharibika kwa mimba. Lakini idadi halisi labda ni kubwa zaidi kwa sababu mimba nyingi hutokea mapema sana katika u

Soma Zaidi...