TATIZO LA UVIMBE KWENYE MATITI (MAZIWA)
Katika hali ya kawaida vimbe nyingi kwenye matiti hazina athari kubwa za kiafya na huondoka zenyewe. Hata hivyo zipo ambazo zinachelewa kuondoka ama haziondoki kabisa. Vimbe hiz huweza kusababishwa na mabo mengi. Lakini zipo chache husababishwa na saratani. Vimbe kwenye matiti mara nyingi si zenye kusababisha maumivu ama kutokwa na majimaji ama maziwa ama damu kwenye chuchu. Je unasumbuliwa na uvimbe wa kwenye matiti, makala hii ni kwa ajili yako.
Sababu za uvimbe kwenye matiti
1.Matiti kujaa majimaji kwenye vijishimo vidigovidogo vilivyomo ndani ya titi
2.Vijitundu vidogovidogo ndani ya titi kujaa maziwa (hutokea wakati wa kunyonyesha)
3.Tishu za kwenye ziwa kuwa kama linyama
4.Majeraha
5.Kuwa na infection (mashambulizi ya bakteria) kwenye titi
6.Saratani ya ziwa
7.Kuota kwa vijinyama kama chunjuwa kwenye mrija wa maziwa
Muda wa kumuona Daktari
Kama ulivyosoma hapo juu kuwa uvimbe wa titi unaweza kuondoka wenyewe bila hata ya kuhitaji dawa. Lakini hutokea ikahitaji kumuona daktari endapo:-
1.Umeingezeka mwingine
2.Uvimbe haukuondoka hata baada ya kupata hedhi
3.Uvimbe unazidi kuwa mkubwa
4.Ziwa limeanza kuonyesha michubuko
5.Ngozi ya ziwa kubadilika rangi
6.Maumbile ya chuchu kubadilika
7.Chuchu kuanza kutoa damu