Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo
1. Kuwepo kwa shinikizo la damu lisilo la kawaida ambapo sio kwa sababu ya mimba ila ni kawaida ya mtu mwenye Ugonjwa huo, kwa hiyo wale wenye Tatizo la shinikizo la damu wanaweza kupata Ugonjwa huu ingawa si wote wenye shinikizo la damu kupatwa na Tatizo hili.
2.pia tatizo hili linawatokea Sana wale wanaobeba mimba za kwanza kuliko wale ambao wamebeba mimba mara nyingi, kwa hiyo wale wa mimba za kwanza wako hatarini kupata Ugonjwa huu.
3.Kwa wale wajawazito wanaopata shinikizo la damu na kiwango cha protini kuwepo kwenye mkojo wakati wa mimba ila wakijifungua tatizo hili linaisha kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba mara wabebapo mimba.
4. Pengine kifafa cha mimba kinakuwepo kwenye familia fulani yaani kuna familia ambazo kila mtu akibeba mimba ni lazima apate kifafa cha mimba, kwa hiyo tunapaswa kufahamu familia zetu na kuchukua hatua mapema ipasavyo hasa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na kupata uangalizi wakati wa ujauzito.
5. Pia ugonjwa huu utegemea na sehemu husika kwa mfano waafrika wanapatwa sana na matatizo haya ukilinganisha na wazungu pamoja na wa hindi mpaka sasa sababu haijawahi kujulikana.
6. Huduma za afya kuwa duni sana, tunasema hivyo kwa sababu kuna wakati mwingine huduma mbaya kwa wanawake huwa chini kwa sababu unakuta wajawazito ni wengi na wahudumu ni wachache hali ambayo Usababisha wajawazito kutopata vipimo vya kutosha, kwa hiyo kama Mama ana tatizo hili ni vigumu kuligundua mapema hali ambayo Usababisha kukuta hali ishakuwa mbaya zaidi ukilinganisha na pale ingegundulika mapema.
7. Watu wenye vitambi.
Kuna utafiti uliobainika kuwa watu wenye vitambi wanapata sana Ugonjwa huu kuliko wale ambao hawana vitambi.kwa hiyo akina Mama wanaotegemea kupata watoto jitahidi kupunguza vitambi ili kuepuka tatizo hili.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Je unasumbuliwa namaumivi wakati wa nlishiriki tendo la ndoa ama baada. Huwenda post hii ikakusaidia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mda ambao mama anapaswa kukaa bila kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto.
Soma Zaidi...Post hii inaenda kufundisha kuhusiana na uvimbe wa kizazi kwa wanawake. Uvimbe wa kizazi no uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao unaweza kuwa ndan ya kizazi uvimbe huu ndan ya mwanamke hujulikana kama (uterine myoma au fibroid). Uvi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wanaotoa hedhi yenye mabonge, ni tatizo ambalo uwakumba wasichana hata wanawake wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake.
Soma Zaidi...Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.
Soma Zaidi...