Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi.
Huduma kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kumfariji mgonjwa na kumpa pole tukijua kuwa sio yeye pekee yake ambaye amepatwa na ugonjwa huu bali ni tatizo la walio wengi na ni la mda maana utokea kwa siku chache na utoweka na kumhakikishia kuwa akibeba mimba hatapata tena tatizo hili
2. Chukua maji ya moto weka kwenye chupa na weka kwenye tumbo lake na maumivu yatapungua na pengine utoweka kabisa na pengine kama hauna chupa chukua kitambaa chochote na weka kwenye maji ya moto ila sio sana kamua na weka kwenye tumbo hasa hasa sehemu ya maumivu na maumivu yatapungua au yataisha kabisa kwa kufanya hivyo mara kwa mara mgonjwa atapata nafuu.
3. Mpatie mgonjwa dawa za kupunguza maumivu kama vile asprin, panadol na dawa hizi zisitumike mara kwa mara zinaweza kusababisha vidonda vya tumbo kwa hiyo wanaovitumia kila mara wawe na tahadhari kubwa kwa sababu matumizi ya mara kwa mara uweza kuleta matatizo makubwa
4. pia mgonjwa anaweza kupatiwa vidonge vya njia za uzazi wa mpango navyo usaidia kupunguza tatizo aina ya vidonge hivi uwa vina homoni ambavyo kwa kitaalamu huitwa combine contraceptive pill, huwa vina homoni zilizochanganywa kwa hiyo msiogope kwamba vina madhara ila upunguza maumivu ya tumbo.
5. Kwa sababu maumivu ya tumbo kama tulivyotangulia kusema kwamba uweza kusababishwa na kuwepo kwa uvimbe kwenye via vya uzazi kwa hiyo ikiwa uvimbe huo umeonekana ni vizuri kumwandaa mgonjwa kwa ajili ya upasuaji ili kuweza kuondoa uvimbe huo ambao unaweza kuleta madhara makubwa zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba na dalili za siku hizo.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Utasa wa Mwanaume hutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume, utendakazi usio wa kawaida wa manii au kuziba kwa manii ambayo huzuia utoaji wa mbegu za kiume. Magonjwa, majeraha, matatizo ya kiafya sugu, u
Soma Zaidi...Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia.
Soma Zaidi...Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu.
Soma Zaidi...Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu.
Soma Zaidi...dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...