Uchafu unaotoka ukeni na rangi zake.

Posti hii inahusu zaidi uchafu unaotoka ukeni na rangi zake, kwa kawaida ukeni utolewa uchafu, uchafu huo unaweza kuwa kawaida na unaweza kuwa na rangi mbalimbali kutokana na kuwepo kwa Maambukizi.

Uchafu kutoka ukeni na rangi zake.

1. Kuna uchafu wenye rangi ya kahawia na uambatana na damu.

Uchafu huu unaweza kutoka kwa wale ambao wanaingia kwenye siku zao za mwezi na wale ambao wameshamaliza, kwa wale wanaoingia kwenye siku zao za mwezi inawezekana ni kubadilika kwa mzunguko ila kwa wale ambao washamaliza inawezekana ika ni kansa ya kizazi.

 

2.Angalizo kwa akina Mama ambao wameshamaliza taratibu za mzunguko wa damu na wakaona tena damu inatoka ni vizuri kuwahi mapema hospitali kwa uchunguzi zaidi ili kuangalia shida ni nini kwa sababu kuna akina Mama wengine wakiona mambo kama hayo wanaficha, sio vizuri kuficha ni lazima kuweka wazi ili kupata msaada zaidi.

 

3. Pia kuna uchafu wenye rangi ya njano ikiambatana na harufu mbaya.

Aina hii ya rangi ya njano na harufu mbaya utokana na kuwepo kwa Magonjwa ya zinaa kwa hiyo mtu akipata anapaswa kutibiwa Magonjwa haya.

 

4. Pengine kuna uchafu mweupe mzito kama jibini hii ni aina ya uchafu ambao hutokea kwa wanawake ambao una maana ya kuwepo kwa mashambulizi ya tangazo kwenye via vya uzazi.

 

5. Kuna na uchafu mwingine unakuwa mweupe  au wa kijivu wenye harufu ya samaki .

Pia uchafu wa aina hiyo unaonyesha juwa kuna Maambukizi ya kandaida kwenye via vya uzazi kwa hiyo ni lazima kupima na kutumia dawa.

 

6 . Kwa hiyo kama tulivyoona aina mbalimbali za uchafu na harufu zake tunapaswa kuziangalia kwa makini na kujua shida ni nini kama hujaelewa vizuri unaweza nkumwona mtaalamu yeyote wa afya ili kuweza kupata msaada zaidi kwa sababu Magonjwa yanayoshambulia sehemu za siri Usababisha madhara mengi ambayo ni kansa na ugumba.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/09/Wednesday - 12:25:40 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 4044


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-