Njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito
Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito, ni mojawapo ya njia ambazo utumiwa na wahudumu wa afya ili kuweza kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito.
Njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito.
1.Njia mojawapo ni ile ya kuwapatia wajawazito dawa za kutumia kwa mwezi mzima, dawa hizo ni ferrous sulphate ambayo ina milligram mia mbili na follic asidi ambayo ina milligram 0.4mg hizi dawa kazi yake ni kuongeza damu kwa wajawazito kwa hiyo ni lazima kwa kila mjamzito kutumia dawa hizi na kuepuka mila na desturi za baadhi ya makabila ambayo yanapingana na matumizi ya dawa hizi.
2.Kupima wingi wa damu kwa kila mwanamke ambaye anaanza mahudhurio ya kwanza kwenye kliniki. Kila mjamzito anapogundulika kuwa ana mimba kitu cha kwanza ni kupima wingi wa damu, akikutwa ana upungufu wa damu anapaswa kupewa dawa au kama kiasi ni kidogo mno anaweza kuongezewa damu kwa hiyo ni vizuri mama wajawazito kupima mara kwa mara wingi wa damu.
3.Kuelimisha watu kujenga vyoo na kutumia vyoo mara kwa mara ili kuweza kuepuka wadudu wanaosababisha minyoo na pia kutumia dawa za minyoo kama vile Mebendazole na Albendazole kwa wanawake kwa hiyo wajawazito wanapaswa kutumia dawa hizi ili kuweza kuepuka hali ya kupunguza damu mwilini.
4. Kujaribu kuzuia magonjwa ambayo yanasababisha upungufu wa damu kama vile Malaria na magonjwa mengine kwa hiyo Mama wajawazito wanapaswa kutumia dawa za SP ipasavyo kwa sababu na Malaria nayo usababisha upungufu wa damu.
5.Pia akina mama wajawazito wanapaswa kutumia vyakula ambavyo vinaongeza damu kama vile mboga za majani, matunda, vyakula vyenye madini ya chuma kwa kufanya hivyo damu ya mama inaweza kuongezeka kwa kawaida ili Mama ajifungua anapaswa kuwa na damu walau 12ml kwenye mwili.
6.Kwa hiyo jamii inapaswa kuwaelimisha watu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza damu kwa wajawazito na pia wajawazito wanapaswa kutumia mboga za majani na vyakula vyenye madini ya chuma kwa hiyo kwa upande wa makabila ambayo uwakataza wanawake wasitumie baadhi ya vyakula kama vile mboga za majani wanapaswa kuacha tabia hiyo kwa sababu damu ni muhimu kwa wajawazito .
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka.
Post hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka mambo haya yanaweza yakawahusu akina Mama wenyewe, familia na jamii kwa ujumla.
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria
Post hii inahusu zaidi dawa ya tetracycline katika kupambana na bakteria,ni mojawapo ya antibiotics au anti bacteria ambayo upambana na bakteria kama tutakavyoona hapo mbeleni.
Soma Zaidi...Dalili za kujifungua
Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.
Soma Zaidi...Dalili za mimba ya siku 4
Unaweza kutaka kujuwa je naweza kupata dalili za mimba baada ya siku nne toka ujauzito kutungwa? ama baada ya siku nne toka kushiriki tendo la ndoa. Makala hii itakwenda kujibu maswali haya na mengineyo.
Soma Zaidi...Maumivu ya mgongo kwa wajawazito: Chanzo chake.
Maumivu ya mgongo ni mojawapo ya changamoto za kawaida zinazowakumba wanawake wengi wakati wa ujauzito. Ingawa mara nyingi ni hali ya kawaida inayotokana na mabadiliko ya mwili, inaweza kuleta usumbufu mkubwa katika maisha ya kila siku. Makala hii inaangazia vyanzo vya maumivu haya na jinsi unavyoweza kuyapunguza ili kupata kipindi cha ujauzito kilicho na utulivu.
Soma Zaidi...