MACHO YANAFAFANUA KUHUSU AFYA:
Macho ya mwanadamu yanaweza kuwa ni malango wa kufahamu afya ya mtu kiakili na kimwili. Kupitia macho p[olisi na wapelelezi wanaweza kufahamu mhalifu ni nani. Kupitia macho daktari anaweza kufahamu matatizo kadhaa katika afya ya mtu. Makala hii itakwenda kukufahamisha ni kwa namna gani macho yako yanaweza kuweka wazi kuhusu afya yako. Hapa tutakwenda kuona macho katika nyanja hizi:-
A.Umbo
B.Rangi
C.Michubuko
D.Na kama kuna vinyama vilivyoota kwenye macho.
Baada ya kusoma makala hii utaweza kufanya uchunguzi kuhusu afya yako wewe mwenyewe kabla hujakwenda hospitali. Unaweza kutumia kioo ama mtu aliye karibu nawe. Makala hii sio kipimo cha mwisho, hakikisha kuwa majibu kuhusu afya yako utayapata kwa daktari.
1.Mzunguruko wa macho. Kama kwenye mzunguko wa macho yako kwa nje kuna uvimbe hii inaweza kuashiria kuwa mtu huyu atakuwa anasumbuliwa na aleji. Pia inaweza kuwa ama infection (mashambulizi ya bakteria) kwenye machi yake. Hali hii pia inaweza kuashiria matatizo kwenye figo. Hali hii inaweza kuandamana na dalili kama macho kuwa mekundu, miwasho kwenye macho, kuvimba kwa macho. Daktari ataweza kupima mkojo wako ili kupata taarifa juu ya afya ya figo.
2.Kope; kope inaweza kuwa ni kioo cha kuonyesha afya ya mtu. Kama kwenye maoteo ya kupe kuna rangi nyekundu huashiria kuwa huwenda mtu anasumbuliwa na ugonjwa wa naemia (upungufu wa damu). dalili kuu ya ugonjwa huu ni kupauka kwa ngozi ya ndani ya kope. Kama mtu atashindwa kufunga na kufunguwa kope zake vyema itaweza kuashiria shida kwenye mfumo wa neva.
3.Mijongeo ya macho; misuli inayotumika katika mijongeo ya macho, (kwenda kulia, kushoto, juu na chini) ina mahusiano moja kwa moja na mfumo wa neva yaani mfumo wa fahamu hivyo kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na ubongo. Sasa endapo mfumo wa fahamu na ubongo utakuwa na matatizo huweza kuathiri misuli hii na kusababisha mtu ,ushindwa kujongesha macho yake kwa ufasaha. Kwa mfamo mtu anaweza kushindwa kupeleka jicho lakoe upande mmoja kama wa kulia ama kushoto.
4.Mahala lilipo jicho lako; jicho lipo kwenye sehemu yake maalumu na linafiti vyema hapo. Sasa wakati mwingine jicho la mtu unaweza kuliona kama limeingia ndani sana ama wengine utaliona limetokeza nje sana. Sasa endapo mtu anasumbuliwa na upungufu wa maji mwilini utakuta macho yeke yameingia ndani. Na endapo macho yake yametokeza nje sana huwenda mtu uyu anasumbuliwa na shida ya tezi ya thyroid.
5.Mboni ya jicho lako; Mara nyingi utaona madaktari wanamulika jicho lako. Kinachoangaliwa ni namna ambavyo mboni ya jicho lako itafanya nini baada ya kumulikwa. Kikawaida mboni inatanuka na kusinyaa kulingana na mwanga ulioifikia. Hivyo endapo jicho lako litashindwa kufanya haya itaonyesha shida kwenye mfumo wa fahamu unaoungana kwenye macho.
6.Ndani ya jicho lako; ndani ya jicho kuzungukia hilo jiduara jeupe unalolioa ambalo ndio jicho kuna vimishipa vingi sana vya damu vimelishikilia. Kwa watu wenye hali mbaya ya shinikizo la juu la damu na wale wenye kisukari huweza kuathiri jisho na kusababisha uoni hafifu. Kufanya uchunguzi wa kina juu ya swala hili kunahitaji ujuzi zaidia, wakati mwingine datkari hutumua kimiminika maalumu ili kulegeza jicho. Dakatari ataweza kuchunguza zadi mpaka sehemu yenye makutano ya neva zinazopelekea taarifa kwenye ubongo
Kama kutakuwa na presha kubwa kwenye fuvu huwenda kutokana na stoke, uvimbe wa ubongo ama maradhi mengine, sehemu ya makutano ya mishipa ya neva (disc) kutakuwa na rangi ya mpaiko na vijimishipa vya damu vitakuwa na rangi ya utofauti.
Umeionaje Makala hii.. ?
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Kama mtu anatokwa na damu za pua, basi juwa kuwa anahitaji huduma ya kwanza.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza jinsi ya kumfanyia huduma ya Kwanza kwa mtu aloanguka kifafa
Soma Zaidi...hatari matokeo ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe kwa muda mfupi. Kunywa pombe haraka kupita kiasi kunaweza kuathiri kupumua kwako, mapigo ya moyo, halijoto ya mwili na kunaweza kusababisha Coma na kifo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za ini, kwa kawaida tunafahamu kwamba ini ni sehemu muhimu kwenye mwili wa binadamu kwa sababu ni.likikosa kufanya kazi yake maisha ya binadamu yanakuwa hatarini kwa sababu mbalimbali.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi matokeo ya maumivu makali , kuna wakati mwingine mgonjwa anapata maumivu makali ya viungo na dawa mbalimbali uweza kutolewa kwa mgonjwa huyo lakini matokeo yake huwa ni kuendelea kwa maumivu kwa hiyo yafuatayo ni matokeo ya maumivu
Soma Zaidi...