dalili za mimba baada ya tendo la ndoa na changa ndani ya wiki moja
Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa
DALILI ZA UJAUZITO BAADA YA TENDO LA NDOA
Je umeshawahi kujiuliza ni zipi zinaweza kuwa dalili za kwanza za ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa? Hakika hili ni swali zuri na hapa niyakujuza majibu yake. Ukweli ni kuwa ni vigumu kuona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa kama hutakuwa makini. Yes inawezekana kuzijuwa ila inahitaji uangalizi wa umakini kabisa. Mwanamke mmoja alishaniambia kuwa yeye ndani ya masaa matano baada ya kufanya tendo la ndoa anaweza kujuwa kama amebeba mimba ama laa. Nilipojaribu kumuuliza alikataa kabisa kunieleza.
Je naweza kuziona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa?
Kabla ya kulijibu swahi hili inapasa kujuwa mabadiliko ya mwili wako kabla ya ujauzito ama kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwanza zingatia mabo haya kabla ya kushiriki tendo la ndoa:-
- Jeoto la mwili wako. Hakikisha unatambuwa vyema kama mwili wako joto lake lipo kiasi gani. Na hakikisha unaweza kutofautisha kati ya joto la homa na joto la kawaida.
- Zingatia majimaji ya kwenye uke wako. Zingatia kama uke wako upo katika majimaji ama upo mkavu. Pia angalia rangi za mashavu ya uke.
- Zingatia tarehe zako. Kabla ya kushiriki tebdo la ndoa hakikisha tarehe zako unazifahamu vyema, pamoja na siku zako za hatari ni lini.
Je nitazijuaje sasa hizo dalili baada ya kuzingatia mambo hayo?
Kujuwa kama umebeba mimba ama laa inaweza kuchukuwa hata wiki moja kuona mabadiliko kwenye mwili wako, mabadiliko haya yataweza kukuambia kwamba huwenda umebebe mimba. Ila pia kuna baadhi ya waanwake wanaweza kuyana mabadiliko hayo mapema kabisa. Ila tambuwa kuwa mabadiliko hayo yote yanaweza kuwa ni vyanzo vya sababu zingine na si ujauzito.
Mabadiliko hayo ni kama:-
- Kuongezeka kwa joto la mwili. Kama ulizingatia vyema joto la mwili wako wakati ukiwa katika siku za hatari linakuwa kubwa kulinganisha ziku za nyuma. Baada ya kushiriki tendo la ndoa angalia je joto litapunguwa ama kuongezeka. Kama litapunguwa baada ya kupita siku za hatari huwenda bado hujabeba ujauzito. Lakini endapo utaona joto halipungui na huwenda likaongezeka hii huonyesha kuwa una mabadiliko kwenye mwili wako ambayo huwenda ni ujauzito. Jifunze pia kutofautisha kati ya homa na joto la kawaida.
- Majimaji kwenye uke na njia ya kuelekea kwenye tumbo la mimba. Kikawaida wakati wa siku za hatari kiasi cha majimaji kwenye uke huongezeka, hii ni kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuweza kubeba mimba. Zinapopita siku za hatari majimaji hupunguwa na hatimaye kurudi hali ya kawaida ya ukavu. Sasa endapo majimaji hayatapunguwa na vinginevyo yakawa yanabadilika na kuwa mazito kuliko hapo mwanzo hii huashiria huwenda amebeba ujauzito.
- Ok sasa zingatia ziku zako za hatari.kama ulishiriki tendo la ndoa katika siku hatari kisha ukaanza kuona mabadiliko kama kutokwa na damu chache iliyo tofauti na hedhi, ama maumivu ya tumbo ya ghafla, ama kichwa kuhisi chepesi mabadiliko kama haya na mengineyo huashiria ujauzito.
- Mabadiliko ya rangi kwenye chuchu na mashavu ya uke yanaweza kuwa n dalili ya ujauzito. Matiti kuuma ama kuwa magumu hii ni katika dalili wanayoiona wengi katka wanawake. Mashavu ya uke hubadilika kuwa na uweuzi ama uwekundu kutokana na mishipa ya damu kuja juu na kupitisha damu kwa wingi maeneo ya chini ili kuandaa ukuaji wa mimba.
NI ZIPI DALILI ZA MWANZO ZA MIMBA KUANZIA SIKU YA KWANZA?
Yes kama tulivyoona hapo juu, mabadiliko hayo sio rahisi kutokea kutoka siku ya kwanza, ila yes mwili huanza kuonyehsa mabadiliko ya ndani punde tu mimba inapoingia, lakini kwa mwanamke kuhusi mabadiliko hayo inaweza kuchukuwa muda. Sasa hapa tutaziona kwa ufupi orodha ya dalili za mimba changa:
- Kuingezeka kwa joto la mwili
- Kuongezeka kwa maimaji ya ukeni
- Kutoka na damu kidogo nyepesi
- Maumivu ya matiti na kujaa ama kuwa magmu
- Mabadiliko ya rangi kwenye matiti na mashavu ya uke
- Kutoziona siku zako
- Kichwa kuwa chepesi
- Maumivu ya kichwa, tumbo na kizunguzungu
- Kichefuchefu na kutapika
- Kukojoa mara kwa mara
- Maumivu ya tumbo
JE KAMA SIO MIMBA NINI KITAKUWA.
Si kila dalili za mimba zinamaanisha ni kweli una ujauzito. Unaweza kuona dalili za mimba lakini ukawa huna. Sababu zinazoweza kupelekea hali hii ni kama:-
- Mabadiliko ya homoni
- Mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye ufumo wa mkojo na mfumo wa uzazi
- Vyakula
- Mazingira
- Maradhi mengineyo yahusuyo mfumo wa uzazi
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Nataka nijue Kuwa njia yakuzuia mimba wakati Wakufany tendo La ndoa
Je ungependa kuijuwa Njia ya kuzuia mimba wakati wa tendo la ndoa?. Posti hii itakwenda kukufundisha ujanja huu.
Soma Zaidi...Sababu za Kukoma hedhi (perimenopause)
Kukoma hedhi hufafanuliwa kuwa hutokea miezi 12 baada ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi na huashiria mwisho wa mizunguko ya hedhi. Kukoma hedhi kunaweza kutokea katika miaka ya 40 au 50. Kukoma hedhi ni mchakato wa asili wa kibaolojia. Ingawa pia in
Soma Zaidi...Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa.
Soma Zaidi...Vitu vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid (majimaji yanayomzungruka mtoto aliyekuwepo tumboni wakati wa ujauzito)
Post hii inahusu zaidi viti vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid, ni jumla ya vitu vyote vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid.
Soma Zaidi...Umuhimu wa uzazi wa mpango
Uzazi wa mpango ni njia inayotumiwa na WA awake na wasichana Ili kupata idadi ya watoto wanaowahitaji na kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Soma Zaidi...