DALILI ZA MIMBA CHANGA
Hapo zamani watu walikuwa wakisubiri kuona tumbo linakuwa ama kuona mwanamke hedhi imekata ndipo waseme kuwa huyu sasa ama mimba. Lakini leo tunaweza kugunduwa mimba mapema sana. Makala hii inakwenda kukujuza dalili za mimba. Dalili hizi zimegawanyika katika makundi kakuu mawili. Kama utakuwa na maoni usiwache kuwasiliana nasi hapo chini.



Dalili za mimba za mwanza toka siku ya 1 mpaka wiki
Hizi ni dalilio ambazo zinaweza kuonekana mapema sana kuliko dalili zingine. Unaweza kuziona dalili hizi siku chache toka kubeba mimba. Wengine huchelewa mapaka wiki inapita na wengine mpaka wiki kadhaa. Dalili hizi ni pamoja na:-




1.Maumivu ya kichwa
2.Kizunguzungu
3.Kichwa kuwa chepesi
4.Maumivu ya tumbo
5.Kutokwa na matone ya damu
6.Moyo kwenda mbio
7.Uchovu.



Si lazima mwanamke azione dalili zote hizo anaweza kuona kadhaa, ama akaona moja tu. Hata hivyo tofauti na kuona matone ya damu kwenye nguo yake ya ndani, dalili zilizobaki sio rahisi kuionz kwa mwanamke ambaye mwili wake umezoea mikikimikiki.



Dalili za mimba changa kuanza wiki ya mbili mapak mwezi
Dalili hizi zinaweza kuendelea miezi kadhaa mpaka pale tumbo litakapoanza kuonekana. Zinaweza kuendelea mapka kukaribia kujifunguwa ama zikakata ila si zote. Dalili hizi ni kama:-




1.Kichefuchefu
2.Kutopata hedhi,
3.Kutokwa na matone ya damu ukeni
4.Maumivu ya tumbo kuongezeka
5.Maumivu ya mgongo na nyonga
6.Uchovu
7.Moyo kwenda mbio
8.Tumbo kukuwa
9.Hasira za papo kwa papo
10.Kukojoa mara kwa mara



Katika kipindi hiki mjamzito anatakiwa awe makini sana kuepuka kula dawa bila ya kushauriana na daktari. Anatakiwa apime vipimo vyote na achukuwe mazoezi ya hapa na pale. Awe karibu sana na watu waliokwisha beba ujauzito wapate kumfundisha baadhi ya yapasayo. Hapa mjamzito anaweza kuwa na hasira, kupenda baadhi ya vitu na kuchukia baadhi ya vitu tofauti na kawaida yake.