Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik
1. Njia ya kwanza ni kuepuka matumizi ya pombe, dawa za kulevya na kuvuta sigara.
Hizi ndizo njia ambazo Usababisha mimba kutoka kwa sababu baadhi ya vilevi ni vikali na kuwepo kwa nicotine usababisha kuharibika kwa mimba.
2. Fanya mazoezi mepesi mepesi.
Kwa kufanya mazoezi hayo usababisha ukuaji mzuri wa kichanga ila mazoezi makubwa makubwa achana nayo hasa kufanyanya kazi nzito ambazo Usababisha mimba kutoka unapaswa kuepukana nayo ili kuweza kuepuka na matatizo ya kutoka mimba.
3. Jikinge na Maambukizi mbalimbali hasa kwenye via vya uzazi.
Wakati wa ujauzito ni vizuri kabisa kujikinga na kuwepo kwa magonjwa kwenye via vya uzazi kwa sababu yanaweza kusababisha maambukizi.na kusababisha mimba kutoka kwa hiyo na siku zote epuka kujamiiana na wanaume wengi au mbalimbali wakati wa ujauzito ili kupunguza magonjwa.
4. Na pia wakati wa ujauzito ni vizuri kuepuka kutumia sabuni za kunukia kusafisha uke daima tumia sabuni ya kawaida kwa sababu kuna hatari ya kuua bakteria wazuri wa kulinda uke na kusababisha Maambukizi kwenye via vya uzazi na kusababisha mimba kutoka.
5. Punguza matumizi ya vyakula visivyofaa.
Kwa kawaida kuna vyakula ambavyo havifai wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha caffeine kwa mfano kahawa na matumizi ya mara kwa mara ya soda .
6. Tumia mlo kamili wakati wa ujauzito.
Kwa kawaida mlo kamili unatakiwa wakati wa ujauzito ni pamoja na vyakula na mboga mboga za majani na pia matumizi ya vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kwa kufanya hivyo tunaweza kupunguza kiwango cha mimba kuharibika.fs
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inazungumzia mama wajawazito Mara tu mama anapohisi kuwa yeye ni mjamzito anashauriwa kuanza clinic.na clinic hizi zinasaidia kuwapatia wakina mama elimu,namna ya kumkinga Mtoto asipatwe na maradhi Kama UKIMWI. Pia mama anapoanza clinic
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili.
Soma Zaidi...Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv
Soma Zaidi...Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia maendeleo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama, zoezi hili ufanyika kila mwezi pale mama anapokuja kwenye mahudhurio kwa kufanya hivyo tunaweza kuja maendeleo ya mtoto kwa kila mwezi.
Soma Zaidi...DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO) Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea njia za asili walizotumia zamani katika kupima ujauzito
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...