Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Mambo muhimu ya kuongea na Mama mjamzito.
1. Maelezo kwa ujumla kuhusu Mama.
Maelezo kwa ujumla kuhusu mama kama vile kuna la mama, mme wake, sehemu anapoishi, miaka yake, kazi yake, kazi ya mwanaume, umri wa mwanaume ,jina mwenyekiti wa kijiji na number ya simu hayo yote uulizwa na mwanamke ili kuweza kujua wazi hali yake ingawa kama kitu chochote kimetokea iwe rahisi kumpata au kuna wanawake wengine ambao huwa wanaacha makusudi kwenye mahudhurio kwa kutumia maelezo kwa ujumla ni rahisi kumpata Mama huyo na kuweza kumpatia huduma za muhimu kwa hiyo ni kuhakikisha kujua hali halisi ya Mama.
2.Kujua juu ya mimba za Mama.
Kwa mama mjamzito akija kwenye mahudhurio ni lazima kujua hali ya mimba zake kwa ujumla kwa mfano mimba aliyonayo ni ya ngapi, amezaa watoto wangapi, je walio hai ni wangapi, ambao wamekufa ni wa ngapi au ni mimba ngapi zimetoka kwa kufanya hivyo tunaweza kuja matatizo aliyo nayo Mama katika kujifungua, kwa mfano kama mimba zimetoka tunaweza kujua chanzo cha kutoka kwa mimba na kupata tiba au kama watoto wanafariki kwa mda fulani tunaweza kujua sababu kwa hiyo kwa watoa huduma wanapaswa kuuliza mama kuhusu mimba zake zikoje na kama kuna tatizo liweze kutatuliwa.
3. Kuhakikisha kuwa Mama anajua miezi ya mimba yake na kujua tarehe ya kujifungua.
Mama akija kwenye mahudhurio anapaswa kujua wazi siku ya kujifungua ambapo mhudumu wa afya ambaye ana ujuzi anaweza kumwesabia Mama kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa mwisho wa kuona siku za ke za mwezi na Mama akishaambiwa siku ya matarajio ya kujifungua anaanza kujiandaa taratibu na akisikia mabadiliko anaweza kwenda hospitali au kituo cha afya, na pia Mama anapaswa kujua wazi mda wa mimba yake ambapo kazi hiyo usaidiwa na mhudumu wa afya kuhakikisha kuwa Mama anajua wazi mda wa mimba yake.
4. Mzio au aleji yoyote kwa dawa na chakula.
Mama anapaswa kuongea na mhudumu wa afya kuhusu mzio wowote wa dawa na vyakula kwa sababu kila mahudhurio mama anapaswa kupewa dawa za minyoo, dawa za kumzuia mtoto hasipatwe na Malaria kwa kitaalamu dawa hizo huitwa sp na pia Mama anapaswa kupewa dawa za kuongeza damu ili akija kujifungua awe na damu ya kutosha , kwa kupewa dawa hizo Mama anapaswa kuwa wazi kama kuna dawa yoyote inayoletea mzio au aleji na kuweza kuibadilisha kwa hiyo tuwe makini kwa kujua mizio ya kila Mama.
5. Kumuuliza Mama kama anatumia vileo na Mambo mengine kama hayo.
Kitu kingine ni kumuuliza kuhusu matumizi ya pombe kali, madawa ya kulevya, na vitu vingine ambavyo utumiwa na wanawake wajawazito ambavyo kwa kitaalamu huitwa PICA vitu hivyo ni kama pembe, kula udongo,kula mkaa na vitu kwa ujumla ambavyo si vyakula vitu hivyo huwa havina faida yoyote kwenye mwili na pia Mama wajawazito wanapaswa kuelewa wazi madhara ya madawa ya kulevya, pombe na sigara kwa watoto na kuachana navyo wakati wa ujauzito.
6. Pia Mama anapaswa kuhimizwa kuhusu chanjo na milo anayoitumia kila siku.
Kwa kawaida tunajua kuwa wajawazito wanapaswa kupata chanjo mbalimbali kama vile Tetunus na vitamini A hizi chanjo umkinga mototo kutokana na magonjwa na pia vitamini A uepusha upofu wa mtoto kwa hiyo Mama anapaswa kupata chanjo ambazo ni za lazima na pia Mama mjamzito anapaswa kula na kushiba vizuri anapaswa kula milo mitano kwa siku kama ifuatavyo, kifungua kinywa cha asubuhi, saa nne au tano anapaswa kupata chochote, chakula cha mchana, saa kumi apate chochote na jioni mlo wa usiku.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...Makala hii itakujuza baadhi ya njia utakaoweza kuzifuata ili kukabiliana na fangasi sehemu za siri kwa wanaume
Soma Zaidi...Kama na wewe una tatizo la kupitiliza siku zako za hedhi hli ya kuwa huna ujauzito, soma post hii ina majibu yako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye via vya uzazi kwa wajawazito, tunajua kuwa Mama akibeba mimba tu kuna mabadiliko utokea katika sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kwa mjamzito huweza kuanaa kuonekana mwanzoni kabisa mwaujauzito, ndani ya mwezi mmoja. Ikabidi si dalili pekee ya kuwa ni mjamzito.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza ishara na dalili ninazoonyesha kuwa mimba ipo hatarini kutoka ama inaweza kuwa imeshatoka.
Soma Zaidi...