Utawezaje kukabiliana na changamoto za ujauzito, je ni zipi changamoto hizo. Hapa nitakujuza.
Ni vyema sana kutambuwa hili, kwani itakusaidia katika klujuwa changamioto za ujauzito. Katika dalili hizi za ujauzito zipo ambazo nio zenye kuendelea. Na katika kuendelea hko wengi katika wajawazito wanapatwa na changamoto kadhaa. Hapa nitakueleza nini cha kufanya.
1.Kichefuchefu
Kichefuchefu kinaweza huweza kuchelewa kujitokeza lakioni kinaweza kuwa ni chenye kuendelea. Kwa baadhi ya wanawake kinaweza kwenda mpka miezi kadhaa mbele, ila kwa wengi kinaweza kukata kufikia wiki ya 28. Hii ni changamoto kwakweli kwa wajawazito. Maana kichefuchefu kinaweza lumkoseshea amani wakati mwingine.hali ya kutema mate, kuhisi kutapika ama kichefuchefu kwa ujumla huwasumbua wajawazito. Wataalamu wanaeleza kuwa hasa chanzo cha kichefuchefu ni mabadiliko ya homoni mwilini. Na huwenda pia kuna sababu nyingine.
Kama utakuwa unasumbuliwa na hali hii fanya hivi. Epuka kukaa maeneo yenye joto sana. Epuka kunywa maji wakati unakula. Tumia tangawizi, kwenye chai ama tafuna. Unaweza kuiweka kama unga ama vipande vidogovidogo. Unaweza kutumia bigjii maalumu kwa ajili ya wajawazito.
2.Maumivu ya tumbo:
Kwa wajawazito maumivu ya tumbo mara kwa mara ni hali ya kawaida na yenye kuendelea. Maumivu haya yanaweza kuchukuwa muda mchache na kuondoka. Pia ni yenye kuvumilika yaani mwanamke anaweza kuendelea kufanya shughuli zake. Ila endapo yatakuwa ni makali sana kutovumilika inaweza kuashiria kuna shida kwenye afya ya mwanamke huyu. Ni vyema kufika kituo cha afya kupata ufafanuzi wa hali.
Katika hali ya maumiovu haya ya tumbo mwanamke anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia zipo tiba mbadala kupunguza maumivu. Ila mwanamke awe makini sana maana anaweza kuingia katika hatari endapo atatumia dawa kiholela.
3.Kutokwa na damu:
Kama ilivyo dalili nyingine huendelea basi si jambo ;la kushangaza kwa mwanamke mjamzito kujikuta nguo yake ya ndani kuwa na vitone vya damu. Damu hii si yenye kuchuruzika ama yenye kutoka kwa wingi kama damu ya hedhi. Endapo mjamzito atakuwa anatokwa na damu nyingi eidha iambatane na maumivu makali ya tumbo ama isiambatane ni vyema awahi kituo cha afya kupata uthibitisho juu ya mabadiliko hayo. Maana wakati mwingimne damu inaweza kuashiria shida katika ujauzito.
4.Mabadiliko katika hisia, matakwa na matamanio katika vyakula na vitu vingine.
Haswa mwanamke anaweza kujishangaa mwenyewe inakuweje hali hii. Mwanamke anaweza kuona kuwa nachukia vitui ama kuna watu anawachukia ghafla. Wakati huo huo anaweza kupenda mtu flani sana. Pia kuna wakati atakuwa anachukia baadhi ya vyakula na vitu vingine. Yaani kwa ufupi ni mabadiliko tu katika saikolojia yake. Huu si ugonjwa hivyo hali hii isimpe mawazo saana mwanamke. Watu walio karibu na wajawazito wawe makini pia maana wanaweza kufanya makosa makubwa kama kumpiga na vinginevyo.
5.Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu.
Yes hii ni changamoto kwa kweli. Hii haiwapati wenye mimba ya miezi ya mwanzo, hali hii hutokea wakati mimba imesha komaa miezi ya mbeleni. Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu kwa wajawazito sio jambao la ajabu. Hali huweza kukaa sawa atakapojifungua. Kama mwanamke anasumbuliwa na hali hii, ahakikishe anapumzika katika maeneo yenye utulivu na yaliyopa yaani aepuke kukaa maeneo yenye joto. Pia aepuke kubvaa nguo za kabana. Aepuke kukaa chini katika mkao mmoja kwa muda mrefu.
6.Kuenda haja ndogo mara kwa mara.
Hii ji changanmoto hasa kwa wale ambao ndio ujauzito wao wa kwanza.Hapa pia kuna wajawazito wanajitahidi kujizuia eti wapunguze kuenda haja ndigo. Hii sio sawa kabisa. Mjamzito anatakiwa anaposikia haja kakaitoe wala asihofu kitu huu si ugonjwa na ni kawaida kabisa. Kwa kuwa moyo wake umeongeza utendaji wa kazi hivyo uchujwaji wa damu ni mkubwa. Kwa maendeleo mema ya afya yake na afya ya ujauzito wake, mjamzito asihofu kitu, aende tu haja.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo tunapaswa kujua au kufahamu kuhusu mbegu za kiume, kwa kuwa mbegu za kiume usaidia katika utungaji wa mimba kwa hiyo ni vizuri kabisa kuzitunza Ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa s
Soma Zaidi...Swali langi ni hiliMama mjamzito anapo hisi uchungu je mtoto huendelea kucheza tumboni?
Soma Zaidi...posti hii inaelezea kuhusiana tatizo la muingiliano wa majimaji ya seli za Mtoto kwenye Damu ya mama mjamzito ambao hujulikana Kama Amniotic Fluid Embolism ni hali adimu lakini mbaya ambayo hutokea wakati Maji ya amniotiki Majimaji ambayo huzunguka mtot
Soma Zaidi...Kipimo chamimba cha mkojo, huonyesha nestory miwili kuwa una mimba, na mmoja kuwa huna mimba. Sasa je ukitokea mmoja umekoleana mwingine hafifu? Endelea na pasti Γ’ΕΒΓ―ΒΈΒ hadi mwisho
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi chanzo cha mvurugiko wa hedhi, Kuna kipindi hedhi uvurugika kabisa, pengine unaweza kupata hedhi mara mbili kwa mwezi au kukosa au pengine siku kuwa zaidi ya tano mpaka Saba au kuwa chache, hali hii utokea kwa sababu mbalimbali tut
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango unavyofanya na mwanaume kushiriki, ni njia ambayo umfanye mwanaume awe mhusika hasa wakati wa kujamiiana.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Unaweza kujiuliza ikiwa inawezekana kupata dalili za ujauzito mchanga kama siku 7 baada ya kudondoshwa kwa yai (DPO yaani Days Past Ovulation).
Soma Zaidi...