Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
SIKU ZA KATARI NA SIKU ZA KUSHIKA MIMBA.
Kila mwanamke ana siku yake ambayo ni hatari zaidi kushika mimba. Siku hii inaweza kufanana na mwanamke mwingine ambaye anafanana naye mahesabu. Hata hivyo wanaweza kutofautiana kutokana na vyakula, maumbile na hali za maisha. Hapa nitakuletea orodha ya siku hatari za mwanamke.
Nini maana ya siku hatari?
Hizi ni siku ambazo mwanamke anakadiriwa kupata ujauzito. Ni mfululizo wa siku ambazo makadirio ya mwanamke kupata ujauzito ni mkubwa kuliko siku nyingine. Kabla ya kuzijuwa siku hizi kwanza hakikisha unajuwa vyema idadi ya siku mwanamke anazokwenda hedhi. Wanawake wanakwenda hedhi ndani ya mzunguruko unaoanzania siku 21 mpaka 35. hii inamaana kuna am,bao siku zao ni nyingi na wengine ni kidogo.
Sasa ni ipi siku hatari kwa mwanamke, siku ambayo mawanamke atapata ujauzito?. siku hii nitakuorodheshea, ila kwanza nataka tu nikujuze kwa ufupi sifa ya siku hiyo. Kwa nini, ni kwa sababu siku hizi zipo nyingi na zote ni hatari kwani zinaweza kuleta mimba. Ila katika hizo ipo ambayo ni hatari zaidi. Siku hiyo ina sifa hizi:-
1.Mwili wa mwanamke katika siku hii utakuwa na joto kulinganisha na siku zilizopita. Kwa urahisi unaweza kugunduwa kama unatumia kipima joto. Ila ukiwa makini unaweza kujigunduwa kama joto lako limepanda. Hakikisha ongezeko hiki ka joto hakiambatani na shida nyingine za kiafya kama maradhi.
2.Uteute unaopatikana kwenye shingo ya kizazi utakuwa umeongezeka na ni wenye kuteleza kama vile majimajiya yai lililopasuliwa. Kama utaingizakidole ndani zaidi ya uke unaweza kuupata kwenye kidole chako.
3.Siku hii hamu ya kushiriki tendo la ndoa nikubwa kuliko siku yingine. Hii haina haja ya kuielezea. Kama mwanamke homoni zake hazina shida basi lakima kutakuwa na siku ambayo atahitaji sana kushiriki ngono kuliko siku nyingine.
Nitaijuwaje siku hatari, ya kupata mimba?
Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--
1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.
2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20
Tumia mfano huu kwa kuitafuta siku yako ya kupata ujauzito. Kama utakuwa na maoni na maswali wasiliana nasi hapo chini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao (kasoro ya moyo ya kuzaliwa) ni hali isiyo ya kawaida katika muundo wa moyo wako unaozaliwa nao. utu uzima. Ingawa maendeleo ya kimatibabu yameboreshwa, watu wazima wengi walio na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa wanaweza wasip
Soma Zaidi...Ujauzito unaweza kutoka kwa sababu nyingi kama maradhi, madawa, vyakula na ajali. Unawezakutoa mimba bila kujuwa amakwakujuwa. Damu kutoka ni moja ya dalili za kutoka kwa mimba hata hivyo maumivu ya tumbo huweza kuandamana na damu hii.
Soma Zaidi...Maumivu yavtumbo huwenda yakachanganya sana, Keane yanahusianana sababu nyingi sana. Kina baadhi ya watu hupata na maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa ama punde tu baada ya kumaliza.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa
Soma Zaidi...Inaweza kutokea ukapima mimbaikawa ipo, na baada ya wiki kadhaa unapima tena haipo. Hali hii unadhani inaweza kusababishwa na nini?
Soma Zaidi...Tendo la ndoa wakati wa siku za hedhi ni halia mbayo jamii nying zinakataza. Katika vitabu vya dini pia haviruhusu, hata ki saikolojia utaona kuwa sio jambo jema. Hata hivyo hapa ninakuletea madhara yake kiafya
Soma Zaidi...Je unawaza nini endapo bikra itatolewa bila wewe kukusudia, je imetolewa kwa njia ya kawaida yaani uume ama ilikuwa ni ajali?
Soma Zaidi...Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni
Soma Zaidi...