Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo

Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini

Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo

Dalili za minyoo, sababu zake na kuiepuka minyoo.



Minyoo ni katika wadudu vimelea vinavyowapa shida watu wengi leo hii. Minyoo sio virusi wala bakteria kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakidhania.minyoo ipo katika makundi meengi na huishi katika maeneo mbalimbali kwenye miili yetu ikiwemo tumbo, ini, utumbo, ubongo na kwenye damu na maeneo mengine. Dalili za minyoo hutofautiana sana kulingana na aina ya minyoo na wapi ipo. Lakini zipo dalili zenye kufanana kwa minyoo wote. Katika makala hii nitakwenda kukujuza baadhi ya dalili za minyoo katika mwili wako, pia tutaona sababu za kupata minyoo, wapi minyoo inapatikana na vipi tutaizuia:-


Utaweza kupata minyoo katika hali zifuatazo:-
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo
5.Kula udongo,
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu



DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
1.Kichefuchefu
2.Kukosa hamu ya kula
3.Maumivu ya tumbo
4.Kupungua uzito
5.Uchovu wa viungo
6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.
8.Kuona damu kwenye kinyesi
9.Tumbo kujaa


Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-


1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
B.Kuwa na alegi
C.Kuwa na homa
D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa


2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
A.Kuwashwa
B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.


3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
A.Kupata homa
B.Kuvimba kwa uso
C.Maumivu ya misuli na kuchoka
D.Maumivu ya kichwa
E.Kutokupenda kupigwa na mwanga
F.Matatizo katika macho (conjuctivist)



NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO
Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo. Njia hizo ni kama :-


1.usile chakula, nyama ana samaki ambaye hajapikwa vyema, ama kula nyama mbichi ama isiyoiva


2.Epuka kugusagusa nyama unapoandaa chakula chako, tenganisha nyama kivyake na vyakula vingine wakati unapoandaa kupika.


3.Safisha vyema vyembo ambavyo vimegusa nyama ambayo haikupikwa


4.Usile mimea ambayo inaishi ndani ya maji yabaridi


5.Usitembee miguu wazi kwenye maeneo machafu ambayo yana kinyesi


6.Safisha vyema kinyesi cha wanyama.


7.Hakikisha unapika vizuri nyama mpaka uhakikishe imewiva vyema,


8.Wanya kung’ata kucha ama kunyonya vidole


9.Hakikisha unaosha kila unachokila kwa maji yaliyo safi na salama.


10.Usafi wa mwili, mavazi na mazingira ni muhimu kwa ajili ya kupambana na minyoo.


11.Kuwacha kabisa kula udongo




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 18326

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba

Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.

Soma Zaidi...
Siku za kupata mimba

Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotoa huduma kwa Mama anayevuja damu baada ya kujifungua

Posti hii inahusu zaidi Madara ya kutomsaidia mama anayetokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Soma Zaidi...
Dalili Za hatari ambayo zinaweza kusababisha ugumba

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba.

Soma Zaidi...
Ni ili sababu ya kutokea kwa tezi dume

Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.

Soma Zaidi...
Ni ipi siku ya kupata ujauzito, na nitajuwaje kama nimepata ujauzito?

Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu

Soma Zaidi...
Je tumbo huanza kukua baada ya mda gan?

Ni Swali kila mjamzito anataka kujiuliza hasa akiwa katika mimba ya kwanza. Wengine wanataka kujuwa ni muda gani anujuwe mavazi makubwa. Kama na wewe unataka kujuwa muda ambao tumbo huwa kubwa, endelea kusoma.

Soma Zaidi...
Malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano

Posti hii inahusu malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano, huduma hii ilianzishwa na WHO na UNICEF mwaka 1990 ili kuweza kuzuia Magonjwa na kuwapatia watoto lishe pamoja na hayo walikuwa na malengo yafuatayo.

Soma Zaidi...