Hatua za ukuwaji was mimba na dalili zake

Hatua za ukuwaji was mimba na dalili zake

Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake

HATUA ZA UKUWAJI WA MIMBA NA DALILI ZAKEUjauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-

1.trimester ya kwanza (first trimester)Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine ama moyo na masikio. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 85 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata hivyo wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.

 

Mabadiliko ya mwili katika kipindi hikiA.UchovuB.Kukosa haja kubwaC.KichefuchefuD.Maumivu ya kichwa

 

Nini hakitakiwi kufanyika katika kipindi hiki?A.Wacha kuvuta sigaraB.Wacha kunywa pombeC.Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktariD.Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatariniE.Punguza kuchwa chai kupitilizaF.Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo

 

2.Trimester ya pili (second trimester)Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza uonekana kwa ambaye anataka kuiona kwenye kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na nyinginezo.

 

Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu itarudi vyema na utawza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hki tumbo litaanza kuonekana kukuwa. Katika kipindi hiki jiepushe sana yafuatayo:-A.Kuvaa nguo za kubanaB.Kuwa na hasira mara kwamara. Yaani jitahidi kkutafuta furaha, kaa na maafiki cheka na furahia.C.Usikibane tumbo hata likiwa kubwa vipi.

 

Katika kipindi hiki unawezakuhisi kuingulia mra kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama ana mafua ama pua zimeziba ila akifina hakuna kitu. Pia anaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.

 

Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambuwa sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.

 

3.Trimester ya tatu (third trimester)Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-A.Anapima mkojo kuangalia protiniB.Atakuwa analkuangalia shinikizo la damu (presha)C.Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtotoD.Atakuwa akipima njia ya uzaziatakuwa acheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.

 

Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 6485

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 web hosting     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Je siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Swali langu ni hili doktaJe siku sahihi yakufanya tendo la ndoa niipi ukipata siku zake za hatari?

Soma Zaidi...
Saratani zinazowasumbua watoto.

Posti hii inahusu zaidi saratani zinazowashambulia watoto. Hizi ni aina mbalimbali za saratani ambazo upenda kuwasumbua watoto ambao ni chini ya umri wa miaka mitano na uleta madhara katika kipindi cha makuzi yao.

Soma Zaidi...
je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?

Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?

Soma Zaidi...
Kaka nasumbuliwa saan na tatizo la kuwasha kwenye kichwa Cha uume Sijui nifanyaje

Je kichwa cha uume wako kinawasha, na je kinatoa majimaji kwenye njia ya mkojo, una muda ganinavtatizo hili. Na je ulishiriki ngono zembe siku za hivi karibuni?

Soma Zaidi...
Huduma kwa mtoto mwenye matatizo ya upumuaji

Posti hii inahusu zaidi huduma kwa mtoto mwenye shida ya kupumua, mtoto kama ana shida ya kupumua tunaangalia dalili kwanza na baadaye tunaweza kutoa huduma kulingana na Dalili.

Soma Zaidi...
Nia za kupima ujauzito ukiwa nyumbani, Njia kuu 10 za kiasili za kupima mimba changa

Kuna njia nyingi zinatajwa zinapima mimba kama chumvi, sukari, mafuta na sabuni. Hata hivyo zipo njia zaidi ya 10 za kiasili za kupima ujauzito. Utajifunza hapa zote

Soma Zaidi...