picha

Dalili za mkojo mchafu na rangi za mkojo na mkojo mchafu

Hapautajifunza rangi kuu za mkojo na dalili zako kiafya, mkojo mchafu na dalili zake

Dalili za mkojo mchafu na rangi za mkojo na mkojo mchafu

MKOJO MCHAFU NA RANGI ZA MKOJO NA MAANA YKE KIAFYA


Mwili wa binadamu ukiuchunguza kwa umakini unamengi ya kushangaza. Unaweza kuijuwa afya ya mtu kwa kuangalia ishara kadhaa na ukajuwa hadi maradhi anayouguwa na aina gani ya vyakula anatumia. Kwa mfano kwa kuangalia rangi za kucha, ngozi, macho, mate na mkojo unaweza kuhuwa mengi sana. Uso na nywele zinaweza kukupa hali halisi ya afya ya mtu. UTI ni katika maradhi yanayoweza kuonekana kwa kupitia uwepo wa mkojo mchafu ama kwa rangi ya mkojo. Katika makala hii tutakwenda kuona mkojo unatueleza nini kuhusu afya. Mkojo ukiwa mchafu ama msafi sana nini humaanishwa hapa. Endelea na makala hii, na usisahau kutembelea tovuti hii mara kwa mara.


Rangi za mkojo mkojo na mkojo mchafu na dalili zake
Kabla ya kuendelea kwnza nataka nifahamishe kuhusu rangi za mkojo. Baada ya kuzijuwa rangi hizi tutaweza kuona sasa nini tunajifunza kuusu afya na tabia ya mtu kwa kupitia kuchunguza rangi hizi za mkojo. Mkojo unaweza kuwa na rangi kadhaa kulingana na vyakula, vinywaji na hali ya afya. Miongoni mwa rangi hizo ni:-


1.Mkojo wa rangi ya njano
2.Mkojo wa rangi ya hudhurungi
3.Mkojo wa rangi nyekundu
4.Mkojo wa rangi ya chungwa
5.Mkojo wa rangi nyeupe
6.Mkojo wa rangi buluu
7.Mkojo wa rangi ya kijani.


Katika hali ya kawaida rangi ya mkojo huanzia kwenye njano. Kuzidi kwa njano inamaana hunywi maji ya kutosha. Na kadiri unavyokunywa maji kwa wingi ndivyo rangi ya mkojo inavyoendelea kusafika. Sasa ikitokea rangi ya mkojo inakuwa tofauti na hivi huwa kuna shaka inaingia. Na endapo unaona damu kwenye mkojo wako hakikisha unafika kituo cha afya maramoja maana utakuwa na tatizo la kiafya linalohitaji msaad haraka iwezekanavyo.


1.Mkojo wa rangi Rangi nyekundu au waridi (pink)
Rangi hii katika mkojo wako sio jambo la kuhamaki saana na ukaanza kuoata hofu. Hata usiwe na hofu saana uonapo rangi njekundu au pink kwenye mkojo wako. Miongoni mwa sababu zinazoweza kupeleke rangi ya mkoj wako kuwa hivi ni:-


A.Damu. Rangi ya mkojo wako kuwa mwekundu inaweza kuwa kuna damu inaingia kwenye mkojo. Damu hii inaweza kuashiria vitu kadhaa ambavyo nu hatari sana kwa afya yako. Kwa mfano kama rangi ya mkojo wako ni nyekundua na pink na ikawa sababu yake ni kuchanganyikana na damu, basi hapa tunaweza kusema kuwa: huwenda mtu huyu ana kichocho, au UTI, korodani linashida, ana mauvimbe yanayosababishwa na saratani, ana shida kwenye figo,amekimbia kwa umbali mrefu na kwa muda mrefu,ana vijiwe kwenye figo ama kwenye kibofu. Kama mkojo una rangi nyekundu hivyo moja kati ya hizo huwenda ndio sababu.


B.Vyakula pia vipo vyakula mtu akila huweza kubadili rangi ya mokojo wake na kuwa mwekundu.


C.Matumizi ya madawa. Yapo baadhi ya madawa yanaweza kubadili rangi ya mkojo kuwa mwekundu ama pink. Kwa mfano dawa kama rifampin ambazo ni antibiotics za kutibu TB.


Hivyo basi kama rangi ya mkojo wako ni nywekundu ama ni pink huwenda moja katika sababu tatu za hapo juu huchangia huenda ni vyakula ama madawa ama mchanganyiko wa damu. Na kama mkojo umechanganyika na damu na kuwa mwekundu ni vyema kwenda kituo cha afya kupata vipimo.


2.Mkojo wa rangi ya chungwa.
Kama ilivyokuwa kwa rangi nyekundu hata rangi ya chungwa kwenye mkojo wako sio jambo la kukupa taabu sanaa. Rangi ya chungwa kwenye mkojo inaweza kuashiria shida za kiafya kulingana na sababu ya kuwepo kwa rangi hiyo. Kwa mfano mkojo wa rangi ya chungwa unaweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-


A.Matumizi ya madwa: madawa huweza kuchangia katika kubadili rangi ya mkojo wako kuwa wa njao. Kwa mfano madawa ya anti-nflammatory kama vile sulfasalazine (Azulfidine) phenazopyridine (phyridium) ama madawa aina za laxatives na baadhi ya madawa ya kufanyia chemotherapy. Madawa haya yanaweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuufanya mkojo wako kuwa wa rangi ya chungwa.


B.Mkojo unaweza kuwa narangi ya chungwa kutokana na sababu za kiafya. Yaani yapo matatizo ya kiafya ukiwa nayo mkojo wako unaweza kuwa ni wa rangi ya chungwa. Kwa mfano mkojo unaweza kuwa wa chungwa kama una shida kwenye ini ama mrija wa nyongo na hali hii huendana na kuwa na kinyesi cha rangi ya mpauko. Pia kama huna maji ya kutosha mwilili hii inaweza kusaabbisha mkojo wako kuwa na rangi ya chungwa.


3.Mkojo wa rangi ya buluu na kijani.
Si jambo la kawaida kuona mkojo wako una rani ya buluu ama kijani. Lakini pia usipatwe na presha kuona lamda unakaribia kufa. Hapana unaweza kuwa na mkojo wa rangi ya buluu ama kijani na usiwe na shida kubwa za kiafya. Kwani rangi hizi kwenye mkojo huweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-


A.Vyakula, hutokea mtu akila baadhi ya vyakula vikapelekea hali hii. Haswa na hivi ndivyo.


B.Matumizi ya madawa. Yapo madawa ukitumia yanakwenda kubadili rangi ya mkojo na kuwa ya buluu ama kijanai. Kwa mfano amitriptyline, indomethacin (Indocin, Tivorbex) na propofol (Diprivan)


C.Pia maradhi. Unaweza kuwa na maradhi yakapelekea rangi ya mkojo kuwa ya buluu ama kijani. Kwa mfamo maradhi yaitwayo hypercalcemia. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuzidi kwa madini ya calcium mwilini. Ugonjwa huu unaweza kuathiri utendaji wa kazi wa kibofu, figo, moyo na ubongo. Pia rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo inaweza kusababishwa na maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.


Huvyo basi punde uonapo rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo wako ni vyema kufika kituo cha afya kujuwa hali yako zaidi. Na ujuwe nini hasa chanzo cha rangi hiyo.


4.Mkojo wa rangi ya hudhurungi
Kama mkojo wako una rangi ya hudhurungi pia usipatwe na presha saana. Rangi ya hudhurungi ni kama rangi tulizotaja hapo juu. Kwenye mkojo rangi ya hudhurungi inaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo:-


A.Vyakula. Kama ilivyo rangi nyengine kwenye mkojo, vyakula huchukuwa nafasi. Kwa mfano zipo aina flani za maharagwe ukitumia rangi ya mkojo wako inaweza kuwa ni ya hudhurungi.


B.Madawa: kuna madawa mengi sana yanayoweza kupelekea rangi ya mkojo wako kuwa ya ahawiya. Kwa mfano madawa ya kutibu malaria (antimalarial drugs) kam vile chloroquine na primaquine, pia madawa ya aina za antibiotics metronidazole (Flagyl) na nitrofurantoin (Furadantin), laxatives containing cascara au senna, na methocarbamol — a muscle relaxant hizi zote huweza kusababisha rangi ya mkojo wako kuwa wa hudhurungi.


C.Pia maradhi, kwa mfano rangi ya mkojo inaweza kuwa ya hudhurungi kama una shida kwenye ini ama figo. Pia maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kusababisha hali hii.


D.Kufanya mazoezi makali kwa muda mrefu.


5.Mkojo wa rangi ya mawingu.
Maambukizi ya njia ya mkojo na mawe ya figo yanaweza kusababisha mkojo kuonekana kuwa wa mawingu.


6.Mkojo mweupe. Kama mkojo wako ni mweupe hongera sana. Inamaana umekunywa maji ya kutosha. Maji uhai, na viungo vyote vinahitaji majiili kufanya kazi vyema. Endapo mwili umepata upungufu wa maji unawez kupata shida za kiafya mwilini.



Kama rangi ya mkojo wako haisababishwi na vyakula basi huwenda ni kwa sababu ya madawa ama mardhi. Hivyo ni wakati sasa wa kujichunguza vyema. Kama umependa makala hii usiwachekutembelea kwenye tofuti hii wakati mwingine upate makala nzuri zaidi ya kiafya.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 5193

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

MATIBABU YA FANGASI

Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi.

Soma Zaidi...
NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA

Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles.

Soma Zaidi...
Dalili za Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (uterine fibroid)

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.

Soma Zaidi...
Dalili za Mgonjwa wa kisukari

Post hii inahusu dalili za mtu Mwenye ugonjwa wa kisukari, dalili hizi zinaweza kujitokeza Moja kwa Moja mtu akagundua kuwa ana Ugonjwa wa kisukari.zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kisukari.

Soma Zaidi...
Nini husababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake na wanaume

Somo hili linakwenda kukueleza vitu vinavyosababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Soma Zaidi...
Dalili za madonda ya koo

Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya koo, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu ya koo la hewa, na na huwa na dalili zake kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Madhara ya kushindwa kupitisha mkojo.

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kushindwa kupitisha mkojo, ni madhara makubwa yanayotokea kwa mtu iwapo akishindwa kupitisha mkojo.

Soma Zaidi...
Maambukizi kwenye uume

Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye uume, maambukizi hata utokea kwenye kichwa Cha uume kwa kitaalamu huitwa Balanitis, zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa ugonjwa huu.

Soma Zaidi...
Tatizo la tezi koo

Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo.

Soma Zaidi...
Matatizo yanayosababisha mshtuko wa moyo.

Mshtuko wa moyo hutokea wakati mtiririko wa damu kwa moyo umezuiwa, mara nyingi kwa mkusanyiko wa mafuta, cholesterol na vitu vingine, ambayo huunda plaque katika mishipa inayolisha moyo (mishipa ya moyo). Mtiririko wa damu ulioingiliwa unaweza kuharibu

Soma Zaidi...