Somo hili ni muendelezo wa pale tulipoishia katika somo lililopita, hapa tutakwenda kusoma Stored Procedure katika MySQL na Tofauti na Function
Kuelewa maana ya Stored Procedure katika MySQL.
Kujifunza jinsi ya kuunda na kutumia Stored Procedures.
Kufahamu tofauti kati ya Stored Procedures na Functions.
Stored Procedure ni seti ya taarifa za SQL ambazo zimehifadhiwa katika database na zinaweza kuitwa ili kutekeleza kazi maalum. Inasaidia kupunguza kurudia rudia kwa misemo (query) ya SQL na kuimarisha utendaji wa database.
Ufanisi: Huandikwa mara moja, inahifadhiwa kwenye server na inaweza kuitwa tena bila kuandika upya.
Usalama: Inaweza kupunguza kiwango cha moja kwa moja cha kuandika SQL kwa watumiaji wa mwisho.
Orodha ya Operesheni: Inasaidia katika operesheni ngumu kama batch processing.
DELIMITER //
CREATE PROCEDURE procedure_name (IN param1 DATATYPE, OUT param2 DATATYPE)
BEGIN
-- Maagizo ya SQL
SELECT column_name INTO param2 FROM table_name WHERE column_name = param1;
END //
DELIMITER ;
Tuseme tunataka kuunda Stored Procedure inayorejesha jumla ya mishahara kutoka kwenye jedwali la employees.
DELIMITER //
CREATE PROCEDURE GetTotalSalary(OUT total_salary DECIMAL(10, 2))
BEGIN
SELECT SUM(salary) INTO total_salary FROM employees;
END //
DELIMITER ;
CALL GetTotalSalary(@salary);
SELECT @salary;
Function ni kipengele cha MySQL ambacho hufanya kazi maalum na mara nyingi hurudisha thamani moja.
Hutumiwa mara nyingi ndani ya queries za SELECT, INSERT, UPDATE, na DELETE.
Ni muhimu kwa kazi za mahesabu au kuendesha data.
CREATE FUNCTION function_name (param1 DATATYPE)
RETURNS DATATYPE
DETERMINISTIC
BEGIN
-- Maagizo ya SQL
RETURN (value);
END;
CREATE FUNCTION GetDiscount(price DECIMAL(10, 2))
RETURNS DECIMAL(10, 2)
DETERMINISTIC
BEGIN
RETURN price * 0.1;
END;
SELECT GetDiscount(500);
Tunakwend akutengeneza table yenye jina la employee na field kama id, na, salary.
CREATE TABLE employees (
id INT AUTO_INCREMENT PRIMARY KEY,
name VARCHAR(100) NOT NULL,
salary DECIMAL(10, 2) NOT NULL
);
Kisha run code hizo hapo chini ili kuingiza data
INSERT INTO employees (name, salary) VALUES
('John Doe', 5000.00),
('Jane Smith', 6200.00),
('Michael Johnson', 4500.00),
('Emily Davis', 7300.00),
('David Wilson', 5400.00),
('Sarah Brown', 4800.00),
('Chris Miller', 6500.00),
('Anna Garcia', 5500.00),
('James Anderson', 5800.00),
('Laura Taylor', 7100.00);
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza database kwenye mysql kwa kutumia interface ya mysql na kwa kutumia sql langauge
Soma Zaidi...Wakati mwingne utahitaji kuwa na function ili kurahisisha uchakataji wa data nyingi bila ya kurudia rudia kuandika code.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kupata orodha ya database, kubadilibjina la database, kufuta database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa data kutoka kwenye database, kwa kudhibiti mpangilio wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza table za database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili jina la table na jina la column kwenye mysql database.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kumalizia program yetu ya kutengeneza matokeo ya wanafunzi kwa kuweka position kwa kila somo na position ya ujumla.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutafuta rank ama position kwenye data base yako kwa kutumia sql. Pia utajifunza kuhusu table alias
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina mbalimbali za database, lugha ya sql pamoja kuzijuwa kazi zake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza nadharia nzima ya view.
Soma Zaidi...