SQL - MySQL somo la 7: Jinsi ya kubadili jina table na column kwenye database
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili jina la table na jina la column kwenye mysql database.
Katika somo lililotangaulia tumejifunza namna ya kutengeneza table. Sasa katika somo hili tutajifunza jinsi ya kuedit jina la table, kufuta. Tutafanya haya kwa kutumia MySQL na kwa kutumia SQL command. Kabla hujaanza somo hili tengeneza table nyingine kisha iite text. Table hiyo ndio tunakwenda kuifanyia mazoezi ya kuiedit jina na kuifuta. Fuata maelekezo ya somo lililotangulia kutengeneza table.
1. Jinsi ya kubadili jina la table kwenye MySQL
Tunabadili jina kwa sababu maalumy, huwenda jina la mwanzo ni gumu sana ama haliendani na data ambazo zipo kwenye database. Ama linafanana na table nyingine ambayo unataka kuitengeneza. Ili kufanya hivi yaani kubadili jina fuata hatuwa zifuatazo:-
1. Tengeneza Table kwa kutumia command hii
CREATE TABLE IF NOT EXISTS test (
id INT,
name VARCHAR (255),
aka VARCHAR (255)
)
2. Bofya hiyo table itafunguka utaona hizo column ambazo umetengeneza.
3. Ingia kwenye operations
4. Kwenda chini hadi ukute palipoandika table options
5. Chini utaona palipoandikwa Rename table to na mbele yake kuna kabox.
6. Kwenye kabox hako weka jina unalotaka lisomeke kwenye table yako mfano tutumie jaribio, hivyo futa jina la mwanzo kisha weka jaribio hapo
7. Bofya GO
8. Mpaka kufika hapo jina la table yako litakuwa limebadilika kuwa jaribio
2. Kubadili jina la table kwa kutumia SQL command
Sasa kama huhitaji kutumia MySQL interface kufanya hivyo unaweza kutumia SQL fuata hatuwa zifuatazo:-
1. Funguwa uwanja wa SQL
2. Kubadili jina tunatumia RENAME TABLE au ALTER TABLE kisha inafatiwa na jina la mwanzo ambalo ni jaribio kisha unaandika to kisha unaweka jina jipya mfano test. Statement hii itakuwa hivi
3. RENAME TABLE jaribio to test;
4. Pia unaweza kutumia hii kubadili jina ALTER TABLE test RENAME to jaribio
5. Baada ya hapo bofya GO
6. Kufikia hapo utakuwa umebadili jina la table yako.
3. Kubadili jina la column
Chukulia unataka kubadili jina la column lmfano katika katika table hiyo tuliotoka kuirename ina column tatui mabzo ni id, name na aka. Sasa tunataka kubadili name tuweke firstname badala ya kuwa nme. Kufanya hivi kwa kutumia MySQL fuata hatuw zifuatazo:-
1. Bofya hiyo table
2. Bofya palipoandika structure
3. Utaona column zote tatu zipo hapo
4. Kwa upande wa kulia kwa kila column kuna palipoandikwa change. Bofya hapo
5. Kutakuja ukurasa wenye vijibox vingi
6. Tafuta kibox kilichoanikwa name
7. Futa name kisha andika jina unalotaka kubadili mfano firstname kumbuka hakuna kuruka nafasi katika kuandika majina.
8. Bofya neno save lipo upande wa kulia
9. Mpaka kufika hapo utakuwa umeweza kubadili jina la column.
10.
4. Kubadili jina la column kwa kutumia SQL
Tofauti na kupitia hatuwa hizo nyingi kwa kutumia SQL unaweza kubadili kwa haraka zaidi. Kufanya hivo fata hatuwa zifuatazo:-
1. Ingia kwenye uwanja wa SQL
2. Kubadili jina tunatumia ALTER TABLE kisha inafata jina la table unalotaka kubadili kisha unaandika neno CHANGE kisha unafata column unayotaka kubadili halafu unafata kuweka jina ambalo unataka iwe, kisha utamaliza na kuandika t...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 web hosting 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Database somo la 25: Utangulizi wa Database ya sqlite
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu aina nyingine ya database inayoitwa sqlite. Hii haihitaji server, na ni faili moja tu.
Soma Zaidi...SQL - somo la 13: Jinsi ya kutumia CASE kwenye SQL
katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutumia case kwenye databse ili kuchakata taarifa za matokeo
Soma Zaidi...SQL - MySQL somo la 1: Jinsi ya kutumia database
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandaa kompyuta ama simu yako kwa ajili ya mafunzo ya database
Soma Zaidi...SQL -MySQL somo la 4; Jinsi ya kufuta database, kuitumia database na kubadili jina la database pamoja
Katika somo hili utajifunza kupata orodha ya database, kubadilibjina la database, kufuta database
Soma Zaidi...Database somo la 22: Primary Key na Foreign Key
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu Primary Key na Foreign Key
Soma Zaidi...SQL somo la 15: Jinsi ya kutumia sql function kwenye mysql
Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function kwenye sql na jinsi ya kuzitumia.
Soma Zaidi...