Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function kwenye sql na jinsi ya kuzitumia.
Katika somo letu hili tutakwenda kufanya mabadiliko kadhaa kwenye database yetu. Hapa tunakwenda kuongeza column ya jina la baba, pia tutaongeza column ya masomo mawili, na ile ya alama tutaibadilisha kuwa somo. hivyo table yetu itakuwa na column hizi:-
kisha weka data kadhaa kama nilivyoweka mimi. angalia picha hapo chini
kufikia hapo utakuw aupo tayari kwa ajili ya somo. kabla hatujaendelea na somo kwanz anikukumbuse kuwa tayari tulisajifunza baadhi ya function kwenye masomo yaliopita kama:-
Katika somo hili tutaendelea kuangalia function nyingineze. Nikukumbushe tu kwanza sql ina mamia fu functions ambazo hatunazizungumzia. hivyo pitaia link hii https://www.w3schools.com/sql/sql_ref_mysql.asp utaweza kusoma function nyingi.
jinsi ya kuunganisha column
Yaani ipo hivi, hapo kwenye column tuna jina la kwanza na jina la pili, ambapo la kwanza ni la mtoto na la pili ni la baba. sasa tunataka watai kwa kusoma hizo column 2 tuzisome kama moja, hivyo basi itatubidi tuziunganishe.
kufanya hivyo tutatumia concat() ambapo ndani yake utaweka hizo column kwa kuzitenganisha na alama ya koma.
Mfano
SELECT concat(jina_la_kwanza, jina_la_pili) as jina FROM majibu;
sasa hapo kuna changamoto tunatakiwa tuzitatue. unaona hapo majina yamebanana, sasa tunataka kuyatengenisha. Ndani ya function ya concat unaweza pia kuunganisha kwa kuweka vitu vingine. Hivyo nitaongeza empty space kwa kutumia (“ “)
SELECT concat(jina_la_kwanza, " ", jina_la_pili) as jina FROM majibu;
Angalau hapo utaona jina la kwanza na la pili vimeachana kitogo.
Kuweka herufi kubwa au ndogo
Wakati mwingine utataka majina yawe katika format moja tu, kwa mfano kama yote yawe na herufi kubwa tupu ama ndogo tupu. Kuwa herufi kubwa utatumia UPPER() na kuwa herufi ndogo utatumia LOWER(). Ndani ya function utaweka jina la column unayotaka data zake ziwe katika herufi kubwa ama nogo.
Mfano:
SELECT concat(UPPER(jina_la_kwanza), " ", UPPER(jina_la_pili)) as jina FROM majibu;
Hivyo hivyo kuwa herufi ndogo utatumia LOWER()
SELECT concat(LOWER(jina_la_kwanza), " ", LOWER(jina_la_pili)) as jina FROM majibu;
...
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutakwenda kumalizia program yetu ya kutengeneza matokeo ya wanafunzi kwa kuweka position kwa kila somo na position ya ujumla.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuunganisha table zaidi ya moja kwneye database.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka kwenye database katika mitindo mbalimbali kama kutoka kubwa kwenda ndogo, ama ndogo kwenda kubwa na mingineyo.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya transaction kwenye database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu Primary Key na Foreign Key
Soma Zaidi...Katika somo ili utakwend akujifunza jinsi ya kuweza kutengeneza variable kwenye database ya mysql
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza table za database
Soma Zaidi...Somo hili ni muendelezo wa pale tulipoishia katika somo lililopita, hapa tutakwenda kusoma Stored Procedure katika MySQL na Tofauti na Function
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili jina la table na jina la column kwenye mysql database.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza nadharia nzima ya view.
Soma Zaidi...