Katika somo hili utakwend akujifunz akuunganisha table zaidi ya moja kwneye database.
Kujiunga kwa jedwali ni mchakato wa kuunganisha data kutoka kwenye jedwali (table) mbili au zaidi kwa kutumia uhusiano uliopo kati ya kolamu zao. Mara nyingi tunajiunga kwa jedwali ili kuchota taarifa ambazo zinahusiana lakini zimetunzwa kwenye jedwali tofauti.
Kuepuka data rudufu: Huwezi kuhifadhi data zote kwenye jedwali moja kwani itasababisha data kurudiwa mara nyingi.
Uhifadhi wa uhusiano: Data zinazohusiana, kama vile bidhaa na wateja walioweka oda, zitatunzwa kwa njia inayoweka uhusiano wazi.
Kuongeza ufanisi: Kupata taarifa sahihi kutoka kwenye chanzo kimoja kilicho na uhusiano ni rahisi zaidi na hupunguza makosa.
Kuboresha muundo wa database kwa kutenganisha data kulingana na aina yake.
Kutoa mwonekano bora wa data zinazohusiana.
Kusaidia katika uchambuzi wa data na kutoa ripoti sahihi.
INNER JOIN: Huchukua rekodi zinazolingana pekee kutoka kwenye jedwali zote.
LEFT JOIN (LEFT OUTER JOIN): Huchukua rekodi zote kutoka jedwali la kushoto hata kama hakuna mechi kwenye jedwali la kulia.
RIGHT JOIN (RIGHT OUTER JOIN): Huchukua rekodi zote kutoka jedwali la kulia hata kama hakuna mechi kwenye jedwali la kushoto.
FULL OUTER JOIN: Huchukua rekodi zote, hata kama hazina mechi kwenye jedwali lingine.
#NB: Katika sql tunatumia alama ya dot ( . ) ili ku refer table ama database husika. Mfano kama table ni duka na ina field kama id, na name , halafu tuna table nyingine bidhaa ina field kama id na name, sasa nikitaka kutumia name kutoka kwenye table duka nitasema duka.name na kama ni name kutoka kwneye table ya bidhaa nitasema bidhaa.name. Hivyo mtindo huu tutakwenda kuutumia zaidi kwneye mifano. Pia katika kuunganisha table tunatumia keyword JOIN ON
Katika somo hili tutakwenda kuunganisha table 3 ili kuweza kufanyia mazoezi namna za kuunganisha table. Table ya duka hii itatunza taarifa za maduka yetu. Chukulia kuwa mtu anawez akuwa na maduka zaidi ya moja, na kila duka likawa na bidhaa ambazo huwenda zisipatikane katika duka lingine.
Table ya pili ni bidhaa, hii itatunza taarifa za bidhaa kama jina la bidhaa pamoja na kuonyesha duka ambalo lina bidhaa iyo. Tutafanya hivi kw akuweka id ya duka hilo.Table ya tatu itatunza taarifa za wateja. Hapa unaweza kuongeza kioengele cha bidhaa walizonunua. Fanya hivi kwa mazoezi zaidi.
-- Jedwali: duka
CREATE TABLE duka (
duka_id INT PRIMARY KEY,
jina_duka VARCHAR(50) NOT NULL,
eneo VARCHAR(50) NOT NULL
);
-- Jedwali: bidhaa
CREATE TABLE bidhaa (
bidhaa_id INT PRIMARY KEY,
jina_bidhaa VARCHAR(50) NOT NULL,
bei DECIMAL(10, 2) NOT NULL,
duka_id INT,
FOREIGN KEY (duka_id) REFERENCES duka(duka_id)
);
-- Jedwali: wateja
CREATE TABLE wateja (
mteja_id INT PRIMARY KEY,
jina_mteja VARCHAR(50) NOT NULL,
simu VARCHAR(15) NOT NULL
);
Sasa kopi code zifuatazo ili kuweka data kwneye table hizo tatu tulizozitengeneza.
INSERT INTO duka (duka_id, jina_duka, eneo) VALUES
(101, 'Duka la Simu', 'Dar es Salaam'),
(102, 'Duka la Kompyuta', 'Arusha'),
(103, 'Duka la Friji', 'Dodoma'),
(104, 'Duka la TV', 'Mwanza'),
(105, 'Duka la Saa', 'Mbeya');
INSERT INTO bidhaa (bidhaa_id, jina_bidhaa, bei, duka_id) VALUES
(1, 'Simu Samsung', 150000.00, 101),
(2, 'Kompyuta Dell', 250000.00, 102),
(3, 'Friji LG', 300000.00, 103),
(4, 'TV Sony', 500000.00, 104),
(5, 'Saa Rolex', 700000.00, 105);
INSERT INTO wateja (mteja_id, jina_mteja, simu) VALUES
(1, 'Halima', '0722000011'),
(2, 'Juma', '0711000022'),
">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya transaction kwenye database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa data kutoka kwenye database, kwa kudhibiti mpangilio wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kumalizia program yetu ya kutengeneza matokeo ya wanafunzi kwa kuweka position kwa kila somo na position ya ujumla.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu nadharia ya Constraints kwenye Database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza database kwenye mysql kwa kutumia interface ya mysql na kwa kutumia sql langauge
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandaa kompyuta ama simu yako kwa ajili ya mafunzo ya database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili jina la table na jina la column kwenye mysql database.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza table za database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu aina nyingine ya database inayoitwa sqlite. Hii haihitaji server, na ni faili moja tu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina mbalimbali za data zinazotumika kwenye mysql database
Soma Zaidi...