Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa data kutoka kwenye database, kwa kudhibiti mpangilio wake.
Katika somo lililotangulia tumejifunza amna a kupangilia taarifa za kwenye databse. Tuliona namna ya kutumia ORDER BY. Isha tukapanga data zetu kutoka kubwa kwenda ndogo na kinyume chake. Sasa katika somo hili tutatkwenda kuendelea na nnamna ya kupangilia data hizo ila kwa kutumia WHERE .
Kwa nini tunatumia where ?
Tunatumia WHERE endapo tuna masharti yanatakiwa yafikiwe ili data kuonekanna. Kwa mfano unataka kusoma menu zote ambazo gharama yake ni zaidi ya 1000. hapa hili tunaita ni sharti ama condition. Sasa ili sharti hili liweze kufanya kazi kwenye SQL tunatumia where.
1. Mfano wa kwanza
Tunahitaji kusoma data zote ambazo price yake ni sawa na 1000.
Kufanya hivyo tutatumia alama ya = mbele ya where. Hivyocommand nzima itaonekana.
SELECT * FROM `menu` WHERE price =1000
hapo menu itakayoonekana ni ile tu ambayo proce yake ni sawa na 1000.
2. Mfano wa pili
Tunataka kusoma data ambazo id yake ni 3, 4, na 8. yaani data tu zenye id hizo ndizo tunataka kuziona na si nyinginezo. Hivyo tunatarajia kuwa na row tatu tu. Kufanya hivyo tutatumia OR kwa maana au. Yaani eidha id iwe 3 au id iwe 4 au id iwe 8. Na command yote itaonekana hivi
SELECT * FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8; pia unweza kuondoa nyota na kupunguza column
SELECT name, price FROM `menu` WHERE id =3 OR id =4 OR id =8;
3. Mafno wa tatu
Chukulia mfano kwenye menu kuna ugali mbili. Kuna ugali nyama abayo ni 1500 na kuna ugali ng’onda ambaypo ji 1000. sasa mimi nataka kusoma ile ambayo ni ugali nyama ya 1500. kumbuka zote ni ugali na kwenye menu zitanasomeka hivyo hivyo. Ili kuona ya ugali 1500 tu tunatakiwa tutumie AND yaani tuselect ugali lakini kwa ulazima kuwa na id yake iwe 1. ambapo kwenye menu yetu id 1 ni ugali hivyo itakuwa hivi:-
SELECT * FROM menu WHERE name = 'ugali' AND id =1
Kuna jambo hapa unatakiwa ulijuwe. Tunapotumia string (sting ni mkusanyiko wa herufi na namba, rejea mafunzo ya php) value inatakiwa ikae ndani ya alama za kufnga na funguwa semi ‘’ kama ulivyo kwenye mfano 'ugali'.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowWakati mwingne utahitaji kuwa na function ili kurahisisha uchakataji wa data nyingi bila ya kurudia rudia kuandika code.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu nadharia ya transaction kwenye database
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kumalizia program yetu ya kutengeneza matokeo ya wanafunzi kwa kuweka position kwa kila somo na position ya ujumla.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kupata orodha ya database, kubadilibjina la database, kufuta database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina mbalimbali za data zinazotumika kwenye mysql database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu Primary Key na Foreign Key
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili jina la table na jina la column kwenye mysql database.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu nadharia ya Constraints kwenye Database
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu aina nyingine ya database inayoitwa sqlite. Hii haihitaji server, na ni faili moja tu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutafuta rank ama position kwenye data base yako kwa kutumia sql. Pia utajifunza kuhusu table alias
Soma Zaidi...