Posti hii inahusu zaidi njia ambazo utumiwa Ili kuweza kuzuia kuwepo ugonjwa wa kisonono, kwa kufuata njia hizi ugonjwa huu wa kisonono unaweza kupungua kwa kiasi au kuisha kabisa.
1. Ili kuweza kuzuia ugonjwa wa kisonono ni vizuri kabisa kujua njia za kusambaa kwa ugonjwa huu ambapo utokea pale mtu mmoja anapojamiiana na mwingine ambaye ana ugonjwa huo bila kutumia kinga kwa hiyo ugonjwa huo utoka kwa mto mmoja kwenda kwa mwingine.
2. Na pia uweza kusambaa wakati mtoto anapozaliwa.
Pale mtoto akitaka kupita kwenye via vya uzazi vya Mama kabla hajatoka nje anaweza kupata ugonjwa huu ikiwa Mama ana ugonjwa wa kisonono, kwa hiyo baada ya kujua njia za kusambaa kwa ugonjwa huu ni vizuri kujua njia za kutibu kama ifuatavyo.
3. Kutumia kondom wakati wa kujamiiana.
Kama una wasiwasi na mpenzi unayejamiiana naye ni vizuri kabisa kutumia kondom, kwa sababu katika matumizi ya kinga wadudu hawawezi kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kujamiiana.
4. Matumizi ya gloves kwa wahudumu wa afya ni muhimu sana.
Kwa Sababu ugonjwa huu kwa wakati mwingine unaweza kutokea kwa kupitia kwenye maji maji, kwa hiyo Mama kama anafanyiwa uchunguzi wa kwenye via vya uzazi Ili kuangalia njia na mambo mengine wakati wa uchungu ni vizuri kutumia gloves Ili kuepuka kuenea kwa ugonjwa huu.
5. Kitu kikubwa na cha maana zaidi ni kiwapima wanawake wajawazito.
Kwa kufanya hivyo ni rahisi kumtambua ni nani mgonjwa na kumwanzishia matibabu au ni nani ambaye sio mgonjwa na kuweza kujikinga zaidi, kwa hiyo ikitokea Mama anaumwa ni vizuri kabisa kumtibu na mwenza wake na wakati wa matibabu waache kujamiiana kwa mda mpaka matibabu yatakapoisha,
6. Kuachana na tabia ya kuchangiana nguo.
Kuna tabia ya watu kuchangiana nguo kama vile chupi na taulo, tabia hii kwa wingi utaikuta kwa wanafunzi wa secondary hasa wasichana wanaoishi kwenye shule za bweni, ni vibaya kwa sababu kama Kuna mwenye ugonjwa huu anaweza akasambaza kwa wengine.
7. Na pia kuachana na tabia ya kutumia via vya uzazi vya bandia, kwa mfano unaweza kukuta mtoto wa kike ana uboo uliotengenezwa kwa bandia akisikia hamu ya kuwa na mwanaume anautumia huo na pia Kuna kipindi anawapatia wengine nao wanaotumia kama Kuna mmoja wapo ana ugonjwa wa kisonono unaweza kukuta wanafunzi wengi Wana ugonjwa huu hata kama wako bweni na hawatoki nje.
8 . Vile vile elimu inapaswa kutolewa kwa wingi kuhusu ugonjwa huu kwa sababu Kuna ambao hawana taarifa kabisa kuhusu kuwepo kwa magonjwa haya, na kwamba yanatibika ni vizuri kabisa kutoa elimu kwa jamii Ili kujua yafuatayo. Njia zinasababisha kuwepo kwa ugonjwa huu, matibabu yake, madhara ya ugonjwa huu na pia namna ya kuepuka ugonjwa huu.
9. Kwa kufanya hivyo jamii itaweza kushutuka na kufuata utaratibu unaofaa Ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama na pia wanawasaidia watoto wadogo kuepukana na kuzaliwa na ugonjwa huu ambapo usababisha magonjwa ya macho kama mtoto amezaliwa nao hata pengine kuwepo kwa upofu kama matibabu hayajafanyika mapema
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia au mbinu ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii, hizi ni njia za awali za kupambana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Bawasili.
Soma Zaidi...Kuvimbiwa kwa watoto ni shida ya kawaida. Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi huonyeshwa na kinyesi kisicho kawaida au kinyesi ngumu na kavu.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wa tishu za matiti kwa wavulana au wanaume, unaosababishwa na kutofautiana kwa homoni za estrojeni na testosterone. Pia unaweza kuathiri matiti moja au zote mbili, wakati mwingine bila usawa. Watoto wachanga,
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kuhusu kushambuliwa kwa moyo na kupumua, kushambuliwa kwa moyo na kupumua kwa kitaala huitwa (cardiopulmonary Arrest) ni kitendo Cha kusimama ghafla kwa moyo na kupumua.
Soma Zaidi...Posti hii inshusiana na dalili za anemia ya minyoo
Soma Zaidi...Dondakoo ni ugonjwa mbaya unaosababishwa na sumu inayotengenezwa na bakteria. Husababisha mipako nene nyuma ya pua au koo ambayo inafanya kuwa ngumu kupumua au kumeza. Inaweza kuwa mauti.
Soma Zaidi...Naomba kuuliza swaliJe mtu anaweza kushiriki mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya ukimwi pasipo kuambukizwa?
Soma Zaidi...Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuangalia sehemu yenye maumivu, hili kugundua mahali mtu anaumia ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya mgonjwa na mhudumu.
Soma Zaidi...