Madhara ya ugonjwa wa ukimwi kwenye jamii.
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.
Madhara ya ugonjwa wa ukimwi kwa jamii.
1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kwamba Ukimwi ni Ugonjwa ambao hauna dawa na umeweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kuleta madhara katika jamii kwa hiyo tunapaswa kujiadhari na ugonjwa huu kwa sababu hauna dawa na unasababisha kifo kwa kuwepo kwa Ugonjwa huu kuna madhara au matokeo hasi yaliyotokana na Ugonjwa huu kama ifuatavyo.
2. Kushuka kwa uchumi wa nchi.
Kwa sababu selikali inatumia hela kubwa kununua vidonge vya kupunguza nguvu za virusi na kutumia pesa kwa kulipa mishahara wafanyakazi wanaohusika na kutoa dawa, na pia kutoa semina mbalimbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kuhamasisha watu wapime na kujua afya zao, kwa kufanya hivyo uchumi unashuka badala ya pesa hizo zingetumika kujenga barabara na shughuli nyingine za kimaendeleo, kwa hiyo kuwepo kwa gonjwa hili kumesababisha kushuka kwa uchumi.
3. Pia kuwepo kwa Ugonjwa huu kumesababisha vifo vya wapendwa wetu,ambapo kumesababisha kuwepo kwa watoto wengi wa mitaani na yatima kila kona kwa sababu ya kutokuwepo mtu wa kuwatunza na kuwapatia mahitaji yao, hali ambayo Usababisha kuongezeka kwa vituo vya watoto yatima na watoto wa mitaani.
4. Vile vie kuwepo kwa Ugonjwa huu kumesababisha kuongezeka kwa Magonjwa mengine kwa sababu kinga ya mwili inaposhuka tu na Magonjwa nyemelezi yanaongezeka kwa hiyo kuna Magonjwa yaliyosababishwa na kushusha kwa immunity kama vile kifua kikuu, kuharisha na magonjwa mengine kama hayo.
5.Kuwepo kwa Ugonjwa huu kumesababisha kuongezeka kwa kiasi cha wagane na wajane kwenye jamii na pia vijana kushambuliwa na Ugonjwa huu na hivyo kupunguza nguvu kazi ya nchi.
6.Kwa hiyo jamii inapaswa kujua Ugonjwa huu na kujiwekea mikakati ili tuweze kupunguza idadi ya Maambukizi kwenye jamii zetu kwa sababu Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Kitau cha Fiqh ๐2 web hosting ๐3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina ๐4 Bongolite - Game zone - Play free game ๐5 ai web app ๐6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Matumizi ya kondom: Njia sahihi ya kujikinga.
โKondomu ni nyenzo yenye ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU), Kaswende, Klamidia, na magonjwa mengine ya zinaa, pamoja na uzazi wa mpango. Ufanisi wake hutegemea kwa kiasi kikubwa matumizi sahihi. Makala hii inatoa maelekezo ya kitaalamu juu ya hatua sahihi za kutumia kondomu, uhifadhi, na mambo ya kuzingatia ili kuhakikisha usalama wa juu.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kisonono, sababu zake nanjia za kujilinda.
Kisonono husababishwa na bakteria. Bakteria ya kisonono mara nyingi hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine wakati wa kujamiiana, ikiwa ni pamoja na kujamiiana kwa mdomo, mkundu au uke.
Soma Zaidi...Dalili za ugonjwa wa UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ugonjwa wa UTI
Soma Zaidi...Je na kwa upande wa mwanaume kuumwa upande wa kushoto wa tumbo kuna shida gani?
Maumivu ya tumbo upande wa kushoti, kwa mwanamke huwenda ikawa ni ujauzito ama shida nyingine za kiafya kama tumbo kujaa gesi, kukosa choo na kadhalika. Sasa vipi kwa wanaume ni ipi hasa sababuรขยโ
Soma Zaidi...Kushambuliwa kwa moyo na kupumua
Post hii inahusu zaidi kuhusu kushambuliwa kwa moyo na kupumua, kushambuliwa kwa moyo na kupumua kwa kitaala huitwa (cardiopulmonary Arrest) ni kitendo Cha kusimama ghafla kwa moyo na kupumua.
Soma Zaidi...