Huduma kwa walio na matatizo ya asili nyingi mwilini

Posti hii inahusu zaidi huduma kwa wale ambao tayari wameshakuwa na tatizo la asidi mwilini, ni njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza tatizo hili au Mgonjwa anapoendelea kupata matibabu.

Mambo ya kufanya kwa walio na tatizo la asidi mwilini.

1. Daima kula chakula kisichokuwa na ubaridi au na moto mwingi kwa hiyo kiwe cha kati na wakati wa kula chakula daima kula chakula kwa utaratibu na meza chakula kidogo kidogo hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda kooni.

 

2. Siku zote usitumie chakula kingi baada ya saa kumi na moja jioni na pia usile chakula na kulala mara tu baada ya kula daima subiri kidogo kabla ya kulala na kula vyakulal laini sana na mlo kidogo baada ya saa kumi na moja jioni.

 

3. Husilale chako baada ya kula,

Kwa kawaida ukimaliza kula Subiri kidogo na ndipo ulale na pia wakati wa kulala daima lala kwa upande usilale chali , ukilala chali unasababisha kiwango cha asidi  kupanda juu na kuingia kooni hali inayoongeza kuwepo kwa tatizo.

 

4. Wakati wa kula kula kiasi kidogo na mara nyingi uwezavyo.

Hii ina maana kwamba siku zota kama umegundua una tatizo hili kula chakula kidogo kidogo na unaweza kutumia mda mwingi yaani kwa siku unaweza kula mala tano ila una kula chakula kidogo kidogo .

 

5. Jaribu kupunguza mfumo wa ulaji.

Hii ina maana kuepuka vyakula vya kukaanga, vyakula vyenye kemikali nyingi na vyakula ambavyo huwa na utamu kinywani ila havina faida yoyote mwilini daima siku zote kama una tatizo hili chemsha chakula chako kwa sababu vyakula vyenye kemikali nyingi na mafuta vina asidi nyingi.

 

6. Epuka nguo za kubana, 

Kwa kawa watu wenye matatizo ya kuwepo na asidi mwilini wanapaswa kuepuka nguo za kubana na kuvaa nguo zilizo wazi ili kuweza kuwa huru na kuruhusu mzunguko wa damu mwilini juwa kawaida



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/03/Friday - 11:50:42 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 724


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-