Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA TENDO LA NDOA
Maumivu wakati wa tendo la ndoa hutokea sana na pengine ni kawaida hasa kwa wanawake. Ijapokuwa kwa wanaume sio sana. Maumivu haya yanaweza kuwa ya tumbo, ya kiuno, ama viungo vya siri yaani uume na uke. Pia maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa tendo la ndoa ama baada.
Je na wewe ni katika wanaopatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Na je umepata kujuwa chanzo cha tatizo lako?. makala hii ni kwa ajili yako. Katika makala hii tutakwenda kuona maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.
1.Mkao uliotumika. Ipo baadhi ya mikao inaongeza uwezekano wa kupatwa na maumivu ya tumbo wakati wa tendo. Mikao hii ni ile ambayo inaruhusu uume kuingia ndani zaidi. Kama unasumbuliwa na tatizo hili jaribu kutumia mikao ambayo utaweza kudhibiti uingiaji wa uume.
2.Kama tumbo la uzazi (uterus) limeinama kidogo. Hii hutokea pale tumbo la uzazi linapolalia nyuma kidogo kuelekea kwenye shingo ya uzazi. Hali hii huwewa kupelekea maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa.
3.Maka una tatizo la kuota tishu zinazopaswa kuota kwenye tumbo la uzazi zikaota sehemu nyingine. Hali hii hutambulika kama endometruisis. Haki hii huweza kupelekea maumivu ya mgongo, nyonga na tumbo wakati wa tendo la ndoa. Dalili za hali hii ni pamoja na:-
A.Maumivu makali zaidi wakati wa tendo la ndoa
B.Kupata hedhi yenye damu nyingi
C.Kutokwa na damu kabla na baada ya kumaiza hedhi
D.Maumivu ya tumbo
4.Kama ovari ina matatizo yaani inajaa maji, hali hii hutambulika kama ovarian cysts. Hii hutokea endapo juu y aovari ama ndani kunkuwa na kama vijifuko vijidogo vinajaa maji. Sasa vikiwa vidogo havinaga maumivu ila vikiwa ni vikubwa vinaweza kupelekea maumivu ya chini ya tumbo. Maumivu haya yanaweza kuwa makali zaidi wakati wa tendola ndoa. Pia mtu anaweza kupata dalili zifuatazo:-
A.Maumivu ya mgongo wa chini ama kwenye mapaja
B.Unahisi tumbo limejaa ama kushiba, ama tumbo linakuwa zito
C.Tumbo kujaa gezi na kucheua gesi kwa mdomoni.
5.Kama kuna mashambulizi kwenye kibofu kitaalamu hali hii huitwa interstial cystitis. Misuli ya kwenye kibofu inashambuliwa na kuvimba na baadaye kutoa dalili kama:-
A.Maumivu ya tumbo na nyonga
B.Kukojoa mara kwa mara
C.Kujihisi kukojoa tena punde baada ya kukojoa
D.Kuvuja kwa mkojo yaani kutoka mkojo bila ya wewe kujuwa.
E.Maumivu kwenye uke na mashavu ya uke (papa)
6.Kuwa na uvimbe kwenye tumbo la mimba kitaalamu huitwa fibroid. Huu ni uvimbe usiosabababishwa na saratani. Uvimbe huuu huweza kuleta dalili kama:-
A.maumivu ya tumbo na mgongo sehemu ya chini
B.Kupata damu nyingi ya hedhi pamoja na maumivu makali
C.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
D.Kukosa choo.
7.Kama mtu ana maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Hapa mtu anaweza kuona dalili kama:-
A.Kutokwa na uchafu ukeni
B.Kutoka na harufu mbaya ukeni
C.Maumivu wakati wa kukojoa na kuhisi kama unaunguwa
D.Maumivu ya tumbo kwa chini pamoja na nyonga
E.Maumivu na kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada ya hedi
8.UTI na PID; kwa pamoja haya ni mashambuizi ya bakteria ama fangasi ama virusi. Mashambulizi haya huathiri mfumo wa uzazi hapa itakuwa na PID na endapo yatashambulia mfumo wa mkojo itakuwa ni UTI. ugonjwa wa UTI na PID huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Dalili za PID
A.Maumivu makali ya nyonga wakatii wa tendo la ndoa
B.Maumivu wakati wa kukojoa
C.Kutokwa na damu wakati wa hedhi na baada
Dalili za UTI
A.Maumivu ya tumbo ambayo huongezeka wakati wa tendo la ndoa
B.Maumivu wakati wa kukojoa
C.Kukojoa mra kwa mara
D.Mkojo mchafu na wenye harufu kali.
9.kama kuna uvimbe katika tezi dume.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika kipindi cha ujauzito, kufanya mazoezi kwa usahihi ni muhimu kwa afya ya mama na mtoto. Mazoezi haya yanasaidia kupunguza uchovu, kudhibiti uzito, kupunguza matatizo ya mgongo, na kuongeza hisia za furaha. Somo hili litatoa mwongozo wa aina za mazoezi zinazofaa kwa kila mwezi wa ujauzito, pamoja na mwongozo wa usalama wa kufanya mazoezi haya nyumbani.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayompata mtu kukosa hamu kabisa ya kushiriki kitendo chochote kinachohusiana na kufanya tendo landoa au bunyeto.
Soma Zaidi...Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili.
Soma Zaidi...Kuuma mwa matiti ni moka ya Ichiro kuwa huwenda ni ujauzito. Hii haimaanishi etindio mjamzito, zipo dalili nyingi za ujauzito. Hata hivyo kuona dalili za ujauzito haimaanishi umepata tayari ujauzito. Kwanza fanya vipimondipo Upate uhakika
Soma Zaidi...Tezi dume hii ni tezi inayopatikana katika katika mfumo wa uzazi wa mwanaume Ila hujulikana kama PROSTATE GLAND. pia hukua karibu na kibofu Cha mkojo na mirija ya mkojo hutumika kuzalisha majimaji (simen) yanayobeba mbegu hivyo bas mk
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uchungu usio wa kawaida kwa akina Mama, kwa kawaida uchungu unapaswa kuwa ndani ya masaa Kumi na mawili ila Kuna wakati mwingine uchungu unaweza kuwa zaidi ya masaa Kumi na mawili na kusababisha madhara yasiyo ya kawaida kwa Mama n
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...