Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

Utajifunza sababua zinazopelekea kuhisi maumivu makali ya tumbo baada ya kumaliza tendo la ndoa

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA
Mara nyingi maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa sio tatizo sana kiasi cha kuogopa. Kwani hali hii husababishwa na gesi iliyoppntumboni mama kama uume ulikuwa ukiingia ndani sana, na hii hutokea endapo uume ni mrefu sana ama mtindo uliotumika katika tendo la ndoa. Tatizo la kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa ama baada hutambulika kama dyspareunia.Inakadiriwa kuwa asilimia 10 mapka 20 ya wanawake huweza kusumbuliwa na tatizo hili. Ila pia tatizo hili si kwa wanawake tu hutokea pia kwa wanaume, ila kwa kiasi kidogo yapata lamda asilimia 5. lakini tatizo hili linatibika bila ya wasi hivyo si vyema kuendelea kuteseka.Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.
Tofauti na sababu ya ya gesi ama uume kuingia ndani sana, tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:-1.Fikra, hisia na mawazo ya mtu. Hii hutokea kama mtu ana misongo ya mawazo kibao, ama ana woga juu ya tendo la ndoa ama mahusianao yake na ya mwenzie sio mazuri lamada amembaka ama kumlazimisha, haya yote yanaweza kutengeneza mazingira ya kuumwa na tumbo baada ya tendo.2.Endapo tendo la ndoa litafanyika kwa kiasi kuwa uume uliingia ndani sana. Hii inaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ila ni ya muda mfupi na yataweza kuondoka baada ya kupumzika. Ni vyema kubadili mikao ama kupunguza kukandamiza sana uume.3.Wakati mwingine hali huweza kutokea endapo mwanamke ameingia kileleni. Wakati wa kufika kileleni misuli inayozungukia mfumo wa uzazi, maeneo ya kiunoni na nyonga misuli hii kusinjaa na kujikaza na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo. Hali jii kitaalamu hufahamika kama dysorgasmia.Watu wanaosumbuliwa sana tatizo hili ni:-
A.Wajawazito
B.Wenye matatizo kwenye ovari
C.wenye mashambulizi ya kwenye mfumo wa uzazi (PID)
D.Wenye matatizo kwenye korodani.4.Gesi; wakati wa kupushi uume ndani unaweza kupushi hewa kuingia ndani ya tumbo. Sasa kama hewa hii itanaswa sehmemu humo ndani inaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa juu ama kifuani. Mtu anaweza kuhisia kama gesi inatembea tumboni na maumivu haya yanaweza kuelekea maeneo mengine ya mwili.5.Kama mtu anasumbuliwa na UTI
UTI inaweza kuwa ni katika sababu za maumivu haya. Mtu pia anaweza kuhisi dalili kama
A.Maumivu wakati wa kukojoa kama anaungua
B.Kukojoa mara kwa mara
C.Mkojo kuwa mchafu
D.Kuwa na damu kwenye mkojo
E.Maumivu ya mkundu.6.Kuwa na maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Pia mtu anaweza kuona dalili kama:
A.Kutoa harufu mbaya sehemu za siri
B.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
C.Maumivu wakati wa kukojoa7.Kama mfuko wa uzazi umeinama, hii inaweza kupelekea kuguswa kwa mfukowa uzazi wakati wa tendo la ndoa hivyo kupelekea maumivu8.Kama kunashida kwenye ovari
9.Kama kuna uvimbe kwenye kizazi. Dalili zake ni kama
A.Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
B.Hedhi kutokata ndani ya siki 7
C.Kukosa choo
D.Maumivu ya miguu ama mgongo10.Kama mirija ya falopia imeziba.11.Kama mwanaume ana maradhi kwenye mfumo wa uzazi.

                   

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2392


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-