picha

Mbinu za kuwakinga watoto na saratani.

Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tun

Mbinu za kupunguza tatizo la saratani kwa watoto.

1.Kwanza kabisa akina Mama wakati wa ujauzito wanapaswa kuhudhuria maudhurio yote ya kliniki ili kuweza kupata mafundisho mbalimbali yanayohusu namna ya kuishi wakati wa ujauzito ili kuweza kupata mtoto ambaye hana matatizo yoyote.

 

2 . Lakini cha kushangaza Mama anaanza mahudhurio ya kliniki mimba ikiwa na miezi sita au saba kusema ukweli hata kama mama anapata mafundisho aameshaharibu kama ni maisha yasiyo ya kawaida kwa mimba ameshafanya na mimba sasa ni kubwa, kwa hiyo akina Mama  mnapaswa kujali  hali  zenu na kutunza watoto wenu vizuri kwa hiyo tuwatunze watoto wetu ili waweze kuwa na afya njema na tushirikiane kuitokomeza janga la saratani kwa watoto wetu.

 

3. Akina Mama wanapaswa kuepuka kabisa matumizi ya sigara wakati wa ujauzito kwasababu moshi wa sigara unaweza kuingia kwenye plasenta na kusababisha maambukizi kwenye sehemu ya plasenta hali ambayo Usababisha kiwango cha kupelekea chakula kutoka kwenye plasenta kwenda kwa mtoto kubwa na hitilafu kubwa hatimaye mtoto uzaliwa akiwa na Dalili za saratani.

 

 4. pia moshi wa sigara usababisha kupunguza kwa vichiocheo vya progesterone na oestrogen na pia katika kufanyika kwa mtoto moshi wa sigara unaweza kusababisha sehemu nyingine kutokamilika vizuri na kusababisha mapungufu kwa mtoto ambayo Usababisha saratani kwa watoto.kwa hiyo akina Mama ni vizuri kuachana na matumizi ya sigara wakati wa ujauzito ili kuweza kumpatia mtoto nafasi ya kukua vizuri akiwa tumboni na akizaliwa awe na afya njema kama watoto wengine.

 

5. Akina mama wanapaswa kukamilisha kwa chanjo za watoto wao, tunajua kubwa chanjo kwa watoto na kwa mama akiwa na mimba ni lazima kuchomwa sindano ya Tetunus kwa ajili ya Mama na mtoto na pia mtoto akizaliwa anapaswa kutumia chanjo zote na kuzimaliza kwa wakati chanjo hizi ni kama vile, chanjo ya kifua kikuu ambayo utolewa kwenye bega la kulia , hii chanjo utolewa tu mtoto anapozaliwa, chanjo ya pili ni chanjo ya polio ambayo uzuia kupooza na utolewa baada ya kuzaliwa, wiki ya sita, wiki ya Kumi mpaka mwisho wiki ya Kumi na nne.

 

6.Chanjo nyingine ni chanjo ya kuzuia kuharisha ambayo kwa kitaalamu huitwa Rotarix ambayo utolewa kwa matone, chanjo hiyo utolewa wiki ya sita na wiki ya Kumi, pia chanjo nyingine ni chanjo inayoitwa pentavalent ambayo inatibu Magonjwa matano Nayo utolewa kwenye wiki ya sita, kumi na kumi na nne, pia chanjo nyingine ni chanjo inayotibu upumuaji na magonjwa ya Nimonia nayo utolewa kwenye wiki ya sita, wiki ya Kumi na wiki ya Kumi na nne na nyingine ni chanjo ya Surua ambayo utolewa kwenye wiki ya nane na kumi na tano, kwa hiyo mtoto akipokea chanjo zote ni mara chache kupata magonjwa ya saratani.

 

7. Kupunguza uharibifu wa hewa kwenye nyumba.

Kwa wakati mwingine mtoto anaweza kupata ugonjwa huu wa saratani kwa sababu ya kuwepo kwa uharibifu wa hewa kwenye nyumba kwa sababu nyumba nyingine unakuta kuna mionzi mikali  na mambo kama hayo ambayo yanaweza kusababisha kuwepo kwa uharibifu kwenye afya wa mtoto , kwa kawaida weka nyumba katika hali ya usafi pamoja na hewa safi.

 

8. Watoto wadogo wasikae Juani kwa mda mrefu.

Tunajua wazi kuwa mionzi ya jua huwa ni hatari kwa kusababisha saratani kwa hiyo ngozi ya watoto wadogo ,inakuwa bado ni raini na zinaweza kupitisha mwanga kwa urahisi kwa hiyo ni vizuri kutowaweka watoto wadogo kwenye  mwanga wa jua kwa sababu ni hatari unaweza kusababisha saratani kwa watoto wadogo.kwa hiyo wazazi wanapaswa kuwaambia wanafamilia wote ili wasiweze kuwapeleka watoto wadogo kwenye mwanga wa jua.

 

9. Mpeleke mtoto mwenye Dalili za saratani hospitali kwa matibabu zaidi.

Kuzama ukweli watu wameshajiwekea imani kubwa saratani hauponi hiyo si kweli kwa sababu saratani ukiwahi pake inapokuwa kwenye hatua za mwanzoni kupona ni rahisi, lakini ukisubiri kwenda hospitalini kwenye dakika za mwisho na za Maambukizi yameshakuwa mengi sana kupona ni vigumu kwa hiyo tunapaswa kuwahi hospitali ili tuweze kupata matibabu mapema.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 1807

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 web hosting     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Dalili za Maambukizi kwenye kitovu cha mtoto

Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal

Soma Zaidi...
Je mjamzito Uchungu ukikata inakuwaje

Hutokea uchungu wa kujifunguwa ukakati. Unadhani ni kitugani kinatokea.

Soma Zaidi...
Dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama mtoto wa kike

Posti hii inakwenda kukueleza jinsi ya kuwjuwa kama mtoto ni wa kike ama wa kiume.

Soma Zaidi...
Imani potofu kuhusu uzazi wa mpango

Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu uzazi wa mpango, ni imani walizonazo Watu kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango.

Soma Zaidi...
Namna ya kufunga kitovu cha mtoto.

Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufunga kitovu cha mtoto mara tu anapozaliwa, kwa kawaida tunafahamu kwamba ili mtoto aweze kuishi akiwa tumboni anategemea sana kula na kufanya shughuli zake kwa kupitia kwenye plasenta kwa hiyo mtoto akizaliwa tu

Soma Zaidi...
Kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi

Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.

Soma Zaidi...