Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum.
3. Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali.
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Utakapofanya ngono na aliyeathirika haimaanishi na wewe kuwa lazima utakuwa umeathirika. Kuathirika kuna mambo mengi lazima yafanyike.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ugonjwa huu uaribu zaidi kwenye mifupa na sehemu nyingine ambazo zinakaribia kwenye mifupa
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu visababishi vya vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Magonjwa ya kuambukiza ni maradhi yanayosababishwa na vijidudu kama vile bakteria, virusi, fangasi au vimelea. Viumbe vingi vinaishi ndani na kwenye miili yetu. Kwa kawaida hazina madhara au hata kusaidia, lakini chini ya hali fulani, baadhi ya viumbe
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ni Maambukizi ambayo hutokea kwenye mifupa kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu ambao hujulikana Kama gangrene inahusu kifo cha tishu za mwili kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu au maambukizi ya bakteria. Ugonjwa wa gangre
Soma Zaidi...