Minyoo Ni nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya minyoo
MINYOO NI NINI?
Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo’ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.
Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii
Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.
Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.
Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).
Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 ai web app 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Dalili za Ugonjwa wa ini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Dalili za kwanza za ugonjwa wa kaswende na kisonono.
Kaswende (Syphilis) na Kisonono (Gonorrhea) ni magonjwa ya zinaa (STIs) yanayoambukizwa kupitia tendo la ndoa. Ingawa husababishwa na vimelea tofauti—Kaswende (bakteria Treponema pallidum) na Kisonono (bakteria Neisseria gonorrhoeae)—yote yanaweza kusababisha madhara makubwa mwilini ikiwa hayatatibiwa mapema. Makala hii inaangazia dalili zao za awali ambazo mtu yeyote anayeshiriki ngono anapaswa kuzifahamu.
Soma Zaidi...Ufahamu ugonjwa wa UTI na dalili zake hasa kwa wajawazito
Wajawazito wanaposumbuliwa na ugonjwa wa UTI, dalili za UTI na namna ya Kujikinga na UTI
Soma Zaidi...Matatizo ya mapigo ya moyo
posti hii inazungumzia kuhusiana na matatizo ya mapigo ya moyo.Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, unaodunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza k
Soma Zaidi...Kwa nini kung’atwa na mbu hakuambukizi UKIMWI?
Ingawa mbu hunyonya damu kwa binadamu, hawana uwezo wa kueneza virusi vya UKIMWI (VVU). Sababu ni kwamba virusi vya VVU haviwezi kuishi wala kuzaliana ndani ya mwili wa mbu, na pia mbu hawaingizi damu ya mtu mmoja kwa mwingine wanapong’ata.
Soma Zaidi...Madhara ya Tiba kemikali kwa wagonjwa wa saratani
Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba kemikali, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wa saratani, madhara haya yanayoweza kuwa ni kwa Sababu mbalimbali kama vile kuaribika kwa seli zinazoendelea kufanya kazi kwenye mwili.
Soma Zaidi...