picha

Vyanzo vya minyoo

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyanzo vya minyoo

VYNZO VYA MINYOO

Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Hapa ninakwenda kukuorodheshea kwa ufupi vyanzo hivi vya minyoo kwa ujumla wao na makundi yao:

 

kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama. Wakati mwingine kuosha tu haitoshelezi, maana unaweza kuosha kwa maji ambayo yana vimelea vya minyoo, hivyo unajikuta hukufanya kitu. Kwani minyoo wanaishi ardhini, kwenye majani na kwenye maji.

Kunywa maji ambayo si masafi na si salama. Maji machafu yanaweza kuwa na mayai ama lava wa minyoo hii. Maji ambayo yamechanganyika na choo kikubwa yanakuwa na mazalia ya minyoo hii. Ni vyema kuchemsha maji hata yachemke, yapozwe na yahifadhiwe vyema kwa matumizi ya nyumbani na hata biashara.

Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi. Upikaji wa nyama yeyote unatakiwa uwe wa makini sana. Kuhakikisha kuwa nyama imewiva vyema. Kuna baadhi ya nyama zinashauriwa kuwa makini sana katika kuzipika kama nyama ya ngurue na ya punda. Pia kuna aiana za samaki nao wanahitajika kuwapika vyema kama samaki aina ya kaa.

Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo. Minyoo huweza kuishi kwenye udongo, na ikitokea my akatembea bila ya viatu katika eneo hili, minyoo hawa wanaweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia mwilini.

Kula udongo, tunaona sana mara nyingi watu wanakula udongo, ukweli ni kuwa sio kila udongo unakuwa na minyoo. Kama utakuwa umeandaliwa vyema unaweza kuwa hauna minyoo. Lakini kula udongo kunaweza kusababisha minyoo. Pia kuna madhara makubwa sana ya kiafya katika kula udongo.

Kinyesi cha wanyama na binadamu. Hivi ni vyanzo vizuri sana vya minyoo. Kwani minyoo wanaweza kuishi kwenye kinyesi vyema na kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo mengine.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021-11-07 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 1651

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 web hosting    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Dalili za mnungu'nguniko wa moyo

Manung'uniko ya moyo ni sauti wakati wa mzunguko wa mapigo ya moyo wako kama vile kutetemeka inayotolewa na damu yenye msukosuko ndani au karibu na moyo wako.

Soma Zaidi...
Tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu (gangrene)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu ambao hujulikana Kama gangrene inahusu kifo cha tishu za mwili kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu au maambukizi ya bakteria. Ugonjwa wa gangre

Soma Zaidi...
Jifunze kuhusu ugonjwa wa bawasiri na dalili zake

Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu ugonjwa wa Bawasiri na dalili zake. Pia utajifunza njia za kujilinda nao.

Soma Zaidi...
Undetectable viral load ni nini?

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya undetectable viral load

Soma Zaidi...
Dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu

Post hii inahusu Zaidi dalili za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu, ni dalili ambazo zinaweza kujitokeza Kwa mgonjwa,Kwa hiyo baada ya kuona dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospital mara moja Kwa ajili ya matibabu.

Soma Zaidi...
Dalili za uti kwa wanaume na wanawake

tambuwa chanzo na dalili za UTI na tiba yake, pamoja na njia za kupambana na UTI

Soma Zaidi...
Zifahmu Dalili za homa ya ini Kali ya pombe.

Posti hii inaonyesha dalili na Mambo Hatari yanayosababisha homa ya ini Kali ya pombe.

Soma Zaidi...
Matibabu ya VVU na UKIMWI

Somo Hili linakwenda kukuletea matibabu ya VVU/UKIMWI

Soma Zaidi...