Dalili za mimba ya watoto mapacha

Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli.

Mapacha hutokea endapo mbegu Mwanamke atatoa mayai mawili na yote yakarutubishwa mapacha wa aina hii ni mapacha ambao hawafanani. Na pia mapacha hutokea endapo yai lililorutubishwa nikajigawa sehemu mbili na kila moja katika sehemu hizo ikakuwa kama mtoto. mapacha wa aina hii hufanana.

 

Dalili za mapacha ni kawaida na zile za mimba za kawaida. hata hivyo kunakuwa na ongezeko la ukali wa dalili hizo. Pia kuna dalili baadhi ambazo hawezi kuzipata mwenye mimba ya mtoto mmoja. Dalili za kawaida za mimba ni kama:

  1. kukosa hedhi
  2. maumivu ya tumbo
  3. kupata kichefuchefu
  4. uchovu
  5. maumivu ya tumbo na kichwa

 

Dalili ambazo ni za kawaida za mimba lakini mwenue mappacha zinaweza kuwa kali zaidi:

  1. Kujaa sana kwa maziwa
  2. maumivu makali ya maziwa
  3. uchovu mkali sana
  4. kuhisi njaa kali na kupata hamu ya kula

 

Tofauti na dalili hizo sasa nitakwenda kukuelekeza daili za mimba mapacha. Hata hivyo dalili hizi zinahitaji kuthibitishwa na kipimo ili kuwa na uhakika kama ni mimba mapacha. Dalili hizo ni kama:-

  1. Mtoto kuanza kucheza mapema sana tofauti na mimba nyingine
  2. Mtoto anapocheza unahizi anacheza kwenye maeneo tofautitofauti ya tumbo na sio sehemu moja.
  3. tumbo huwa kubwa zaidi na hukuwa kwa haraka sana.
  4. kuongezeka kwa uzito haraka haraka
  5. mapigo ya moyo ya mtoto huwa ni zaidi ya mapigo ya mtoto mmoja.

 

Changamoto za mimba mapacha

Mwanamke mwenye mimba ya mapacha anaweza kupatwa na changamoto ambazo zinaweza kuwa kali zaidi ya asiye na mpacha. Changamoto hizo ni kama:-

  1. ongezeko la shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) wakati wa ujauzito
  2. Yupo hatarini kupata kisukari cha mimba
  3. uchache wa majimaji ya amniotic fluid
  4. kujifunguwa watoto njiti
  5. kupasuka kwa placenter

 

Changamoto za mimba mapacha sio tu sitaishia kwa mama bali pia zinaweza kumpata mtoto ama watoto. Matatizo yanayoweza kuwapata watoto ni pamoja na:-

  1. Ubongo kuvuja damu
  2. Kuzaliwa njiti
  3. kuzaliwa na uzito kidogo
  4. kuwa na tatizo la kupata baridi
  5. mtoto kushundwa kula
  6. mtoto kupata matatizo ya kuona

 

Nini kifanyike kumlinda mama na watoto

Kutokana na changamoto ambazo mama mwenye mimba mapacha anaweza kuyapata ama matatizo ambayo yanaweza kuwapata watoto, hapa nitakupa mambo ya kufanya kukabiliana na shida hizo:-

  1. kuhudhuria clinic kila inapofika tarehe ya kwenda bila kukosa
  2. onana na daktari kila unapopata tatizo la kiafya.
  3. kula vizuri
  4. pata muda wa kuoumzika
  5. fanya mazoezi hata ya kutembea
  6. kunywa maji mengi
  7. kuwa na furaha. epuka mambo ya kukuletea misongo ya mawazo.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/03/28/Tuesday - 02:38:36 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 11192

Post zifazofanana:-

Ndege kwenye ulimbo
Wahenga wanaelewa, enzi hizo unaambiwa ndege akinasa basi unakumbuka macho juu asije akayoke. Hukuchinib. hujali kama kuna mjimba ama nini Soma Zaidi...

Dalili za mimba ya watoto mapacha
Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli. Soma Zaidi...

Malezi ya mtoto mchanga na mama mjamzito
Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga Soma Zaidi...