Dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama mtoto wa kike
Posti hii inakwenda kukueleza jinsi ya kuwjuwa kama mtoto ni wa kike ama wa kiume.
Kila mwanamke mwenye mina ana hamu ya mujuwa jinsia ya mtoto wake. Huwenda ili aweze kujiandaa kununua mavazi mapema, ama kupata pongezi kutoka kwa mwenzi wake ambaye amemuahidi kuzipata endapo atakuwa na mtoto wa jinsia fulani. Dalili za mimba iwe ya mtoto wa kike ama wa kiume ni zilezile isipokuwa kuna mambo flani yanaongezeka. Katika post hii nitakueleza dalili ambazo watu wengi wanaamini kuwa zinaonyesha jinsia ya mtoto. Hata hivyo pia nitakueleza usahihi wa maoni yao kitaalamu.
Dalili za kawaida za ujauzito wa mtoto bila kujali jinsia:
- Kutoka na matone ya damu iliyo nyepesi
- Kukosa hedhi
- Maumivu ya kichwa bila ya sababu
- Mwili kuongezeka joto
- Mapigo ya moyo kuongezeka
- Kupata kizungzungu
- Kupatwa na kichefuchefu
- Kuchoka bila ya kufanya kazi
- Maumivu ya tumbo
Sasa wacha tuje kwenye swali letu la awali kuhusu dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama wa kike. katika kuelezea kkila dalili nitakwenda kukuambia uhakika wa dalili hizo. Jambo la kuzingatia ni kuwa dalili pekee hazithibitishi bila ya kupata vipimo kwa kitaalamu. kwani misingi ya dalili hizo imewekwa kutokana na imani za watu vile wanavyodhani ama mazoea yao ama historia ya yale yaliowakuta.
Dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama wa kike:
- Uzito wa tumbo; Inaaminika kuwa endapo mjamzito atahisi tumbo ni zito sana basi mtoto ni wa kiume. lakini endapo tumbo siuo zito sana basi mtoto ni wa kike. Wanaamini kuwa mtoto wa kiume ni mzito kuliko wa kike. Hata hivyo nadharia hii haina uithibitisho wa kitaalamu ijapokuwa watu wanaamini hivyo.
- Kichefuchefu: Wanadai wamama kuwa endapo mjamzito atakuwa na kichefuchefu sana basi mtot ni wa kiume. na endapo hatapata kabisa ama itakuwa ni cha kawaida basi mtoto ni wa kike.
- Mabadiliko kwenye ngozi: Dhana hii ni kuwa endapo mwanamke atapata mabadiliko kwenye ngozi yake, mabadiliko ambayo yatakwenda kuharibu muonekano wa ngozi na uzuri wake basi mimba hiyo ni ya mtoto wa kike. Pia wnaamini kuwa mtoto wa kike anachukuwa urembo wa mama yake. Miongoni mwa mabbadiliko hayo ni chunusi, ngozi kupauka na kukosa mvuto. Kwa uoande mwiungine mtoto wa kiume hawezi kumfanya majamzito abadilikwe na ngazi yake. pia nadharia hii haina ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa madaktari.
- Mabadiliko ya nywele waumini wa dhana hii wanasema kuwa mtoto wa kiume hana shida na uzuri wa mama yake. Kwa kuwa nywele ni moja ya uzuri wa mama basi zitabaki kama zilivyo. kwanamke hatakuwa na mabadiliko ya nywele akiwa na mimba ya mtoto wa kiume. Kwa upande mwingine mimba ya mtoto wa kike itamfanya nywele kunyonyoka ama kukatika. Imani hii pia haina ushahidi wa kisayansi.
- Kuchaguwa sukari na chumvi: Inaaminika kuwa mwanamke mwenye mimba ya mtoto wa kike anapenda sana vitu vitamu. lakini ikiwa mimba ni ya mtoto wa kiume anapendelea sana vitu vyenye chumvi chumvi. hata hivyo hakuna ushahidi wa kitaalamu kuthibitisha nadharia hii.
- Utofauti wa kwenye mapigo ya moyo: Wanaamini kuwa endapo mimba ni ya mtoto wa kike mapigo ya moyo huwa mengi zaidi. kwa mfano yakiwa ni zaidi ya 140 ndani ya dakika basi mimba ni ya mtoto wa kike. na yakiwa chini ya 140 mtoto ni wa kiume. nadharia hii inaonekana ni ya kitaalamu zaidi, hata hivyo haina ushahidi wa kuthibitisha.
Je nitajuwaje kwa uhakika kuwa mtoto ni wa kiume ama wa kike?
Sasa wacha tuangaie kitaalamu zaidi kwa namna gani utaweza kujuwa jinsia ya mtoto. Ukweli ni kwamba utaweza kuwa na uhakika wa jinsia ya mtoto kwa kutumia vipimo. Hivyo hapa nitakueleza baadhi ya vipimo ambavyo vinatumika kujuwa jinsia ya mtoto.
- Kwa kutumia kipimo cha damu cha DNA kwa mfano kipimo cha panorama kinachojulikana kama Noninvasive prenatal testing (NIPT). Kipimo hiki kinaweza kuonyesha jinsia ya mtoto kuanzia wiki ya 7 hadi ya 10 toka ujauzito kutungwa.
- Kwa kutumia kipimo cha utrasound: Kipimo cha utrasound hutumika kumulika ndani ya tumbo la mjaozito na kumuona mtoto na jinsia yake. kipimo hilki kinaweza kuona jinsia ya mtoto kuanzia ujauzito wa wiki ya 18 hadi 20.
Mwisho nimalizie kusema kuwa bila ya kutumia vipimo vya kitaalamu hatuwezi kuwa na uhakika juu y jinsia ya mtoto. Hivyo kwa mwenye kutaka kujuwa jinsia ya mtoto afanye vipimo vya kitaalamu. kwa mfano kipimo cha utrasound sio cha ghali kukifanya ukilinganisha vipimo vinginevyo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Dalili za kupasuka kondo la nyuma (placenta)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kupasuka kwa kondo la nyuma (plasenta) (abruptio placentae) ni tatizo lisilo la kawaida lakini kubwa la ujauzito.Kondo la nyuma (Placenta) ni muundo ambao hukua ndani ya uterasi wakati wa ujauzito ili kumlisha mtoto ana
Soma Zaidi...Dalili za kujifunguwa, na dalili za uchungu wa kujifunguwa
Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...SABABU ZA KUKOSA NGUVU ZA KIUME AMA KUWA NA UWEZO MDOGO WA KUHIMILI TENDO LA NDOA
Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Sababu za mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Njia za uzazi wa mpango kwa akina Mama kuanzia miezi sita baada ya kujifungua mpaka mwaka mmoja
Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa mama aliyejifungua kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Soma Zaidi...Je chuchu zikiwa nyeusi Nini kinasababisha,, kando ya kuwa mjamzito? Na Kama sio mjamzito sababu ya chuchu kua nyeusi ni nini
Chuchu kubadilika range ni mojavkatika mabadiliko ambayo huwapa shoka wengi katika wasichana. Lucinda nikwambie tu kuwa katika hali ya kawaida hilo sio tatizo kiafya.
Soma Zaidi...