Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mimba iliyotunga nje na madhara yake kiafya
MIMBA ILIYOTUNGIA NJE:
Mimba ya namna hii kitaalamu hufahamika kama ectopic pregnancy. Je hii ni mimba gani? Hii ni mimba ambayo yai lililorutubishwa linaendelea kukuwa nje ya mji wa mimba (uterus). mimba inaweza kukuwa sehemu yeyote kwenye tumbo ila nje ya mji wa mimba. Kwa asilimia kama 90% mimba hukuwa kwenye mirija ya falopia. Hii ni mimba hatari sana na inahitaji uangalizi wa haraka sana, kwani inaweza kuhatarisha maisha ya mama. Inakadiriwa kuwa mimba za namna hii huchukuwa kati ya asilimia 1 mpaka 2 ya miba zote.
Kwa nini mimba hii ni hatari?1.Mimba inatkuwa nje ya mji wa mimba hivyo haiwezekani mtoto kupona2.Inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ama sehemu ilipokuwa.3.Inaweza kusababisha ulemavu kwa mama endapo itachelewa kuonekana4.Kwa asilimia 30 mimba hii haina dalili hii ni hatari zaidi.5.Inaweza kusababisha uvujaji wa damu kwa kiasi ikubwa6.Inaweza kusababisha mwanamke kuhitajiwa kufanyiwa upasuaji kamma tiba.
Sababu za kutokea mimba hiiKama nilivyotangulia kukueleza kuwa asilimia 30 ya mimba hizi hazina dalili. Lakini kwa kiasi kikubwa mimba hizi huwa na dalili. Tafiti zinaonyesha kuwa dalili zake hutokea kabla ya wiki ya 10. Sasa hapa nitakutajia baadhi tu ya dalili za mimba hii:-1.Maumivu ya tumbo upande mmoja wa nyonga.2.Maumivu ya mabega3.Kutokwa na damu kwenye uke.4.Maumivu ya nyonga.5.Mvurugiko wa tumbo na kutapika6.Maumivu ya upande mmoja wa mwili.7.Kizunguzungu na uchovu8.Maumivu ya mabega, shingo na mkundu.
Sababu za kutokea kwa mimba hii.1.Kuwa na maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID2.Uvutaji wa sigara3.Kama una umri wa miaka 35 na kuendelea4.Kama unatumia madawa ya kuivisha mayai5.Kama ulishapata ujauzito huu hapo mwanzo upo uwezekano kuja kupata tena6.Kama ulifanyiwa upasuaji kwenye mirija ya falopia7.Kama una tatizo la endometriosis8.Baadhi ya njia za kuthibiti uzazi mfano, IUD
Nini tena yapasa kujuwa?1.Ujauzito uliotungia njea haurithiwi yaani kama mama aliwahikupata ujauzito huu hali hii hairithiwi.2.Kutoka kwa ujauzito sio sababu ya kupata mimba hii3.Kutoa ujauzito pia hakuna mahusianao na ujauzito huu4.Mazoezi na michezo pia hihusiani na kutokea kwa ujauzito huu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mambo anyopaswa kujua akiwa mjamzito. Ni mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama akiwa mjamzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za mimba inayotaka kutoka yenyewe, Kuna wakati mwingine mama anabeba mimba na mimba hiyo I atishia kutoka na huwa inaonyesha dalili mbalimbali kwa hiyo zifuatazo ni dalili za mimba kutaka kutoka yenyewe.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza homoni za kiume kwa akina dada.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa namaumivi wakati wa nlishiriki tendo la ndoa ama baada. Huwenda post hii ikakusaidia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.
Soma Zaidi...