picha

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula

Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA KULA




Baada ya kula ni wakatiwa wa kupumzika, lakini sivyo kwa baadhi ya watu. Wao anapomaliza tu, anangojewa na maumivu ya tumbo. Je unajuwa sababu?, je na wewe unapatwa na maumivu ya tumbo baada ya kumaliza kula? Makala hii ni kwa ajilli yako.



Kwa ufupi maumivu haya yanaweza kusababishwa na mchafuko wa tumbo. Tunapozungumzia mchafuko wa tumbo tunazungumzia mmeng’enypo wa chakula unakuwa na hali ambayo si ya kawaida.



Dalili za mchafuko wa tumbo ni kama:-
A.Kichefuchefu
B.Kuhara
C.Kiungulia ama kucheua
D.Kujaa tumbo na kutoa hewa kwa mdomoni. Kwa kucheua
E.Maumivu ya tumbo
F.Kushiba kusikkokuwa kwa kawaida
G.Lushiba kwa haraka
H.Maumivu ya sehemu ya juu ya tumbo
I.Kuhisi kuunguwa chini ya tumbo
J.Kuhisi kuunguwa kifuani na maumivu ya kifua
K.Kutapika




Nini husababisha maumivu ya tumbo baada ya kula?
Kwa hakika kuna sababi nyingi ambazo zinaweza kupelekea maumivu ya tumbo baada ya kula. Sio hivyo tu pia tumbo linapatwa na machafuko makubwa kwa mfano kutapika, kichefuchefu, kuharisha na mengineyo. Sasa ni zipi sababi hizo zinazoletwa maumivu ya tumbo baada ya kula?



1.Aleji ya chakula.
2.kuna baadhi ya vyakula huwa vina aleji, hii hutokea pale mwili mwili unapokidhania chakula kuwa hakipo salama, na kuanza kukishambulia ili kukitoa. Hali hii hupelekea maumivu ya tumbo kama matokeo ya mpambano. Baadhi ya vyakula vyenye aleji ni kama:-
1.Maziwa
2.Maharagwe ya soya
3.Baadhi ya samaki
4.Vyakula jamii ya karanga na korosho
5.Mayai
6.Ngano



3.kama mfumo wa kumeng’enya chakula umeshindwa kukivumilia aina ya chakula ulichokula. Yaani mfumo wa chakula unashindwa kukimeng’enya kabisa ama kinameng’enywa lakini si kwa ufasaha. Kwa mfano baadhi ya vyakula vilivyotengenezwa na maziwa kwa baadhi ya watu inakuwa ni tatizo na hupelekea mvurugiko wa tumbo.



4.kama ukuta wa utumbo mdogo umeathiriwa na protini ya gluten, protini inayopatikamna kwenye nafaka kama ngano na shayiri. Hali hii hutambulika kama celiac disease.



5.Kama una tatizo la kupanda kwa tinikali za tumboni kuja juumkwenye koo sehemu inayojulikana kama esophagus. Tindikali hii inaweza kuathiri kuta za kiungo hiki na kusababisha machafuko ya tumbo. Hali hii kitaalamu hutambulika kama Gastroesophageal disease (GERD)



6.kama una matatizo kwenye utumbo mkubwa kwa kitaalamu huitwa irritable bowel syndrome. Hali hiii inaweza kuonyesha dalili kama:-
A. Maumivu ya tumbo
B.Kujaa kwa tumbo
C.Kuharisha
D.Kukosa choo
E.Kujaa gesi



7.Kuvimba kwa baadhi ya sehemu kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Mgonjwa anaweza kuona dalili kama maumivu ya tumbo, kuhara, damu kwenye kinyesi n.k



8.Kama una vidonda vya tumbo. Vidond vya tumbo vinaweza kusababisha maumivu ya tumbo baada ya kumaliza kula.



9.Kukosa choo. Hali hii hutokea pale chakula kinapotembea kidogokidogo katika njia ya mmeng’enyo wa chakula.



Namna ya kujikinga na maumivu ya tumbo baada ya kula.
1.Kama kuna chakula unakumbuka kilikuletea matatizo kama haya hebu kiepuke
2.Kula chakula chenye kambakmba kwa wingi na matunda
3.Kunywa maji mengi
4.Punguza unywaji wa pombe
5.Punguza matumizi ya caffein (majani ya chai kwa wingi)
6.Punguza misongo ya mawazo





                   



Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 5087

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Orodha ya madini, chanzo chake na faida zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula nyama

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama

Soma Zaidi...
UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuboresha afya ya meno

Katika post hii utakwenda kujifunza vyakula unavyopasa kul ili kuboresha afya ya meno yako. Pia utajifunza vyakula vilivyo hatari kwa afya ya meno yako.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple

Soma Zaidi...
Vyakula vya madini, kazizake na athari za upungufu wa madini mwilini

Je ungependa kujuwa vyakula hivyo ama vyanzo vya madini? Na je ungependa kujuwa ni zipi hasa kazi za madini katika miili yetu?. makala hii ni kwa ajili yako, hapa utakwenda kujifunza mengi kuhusu somo hili.

Soma Zaidi...