Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia
FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA BAMIA (OKRA)
Bamia ni katika matunda ambayo ni mboga na karibia maeneo mengi mboga hii inapatikana. Bamia ni katika mboga muhimu sana kwani ina faida nyingi sana. Ndani ya bamia kuna vitamin, madini na kambakamba. Bamia hutumiwa kuanzia majani, mbegu, bamia lenyewe , maua, kikonyo na matawi. Kwa ufupi mbamia wote ni mboga na huliwa.
Ndani ya bamia kuna fiber (kambakamba), folate, vitamin K na madini. Bamia husaidia katika kuboresha na kuimarisha afya ya moyo pia hulinda mwili dhini ya saratani. Jitahidi ukinunua bamia lisikae zaidi ya siku tatu ama nne. Madini ya potassium na sodium hupatikana katika bamia bila ya kusahau vitamin A ambavyo hupatikana pia kwenye bamia.
Ndani ya bamia kuna aina ya protin inayoitwa lectin, ambayo pia huweza kupatikana kwenye maharage na nafaka nyingine. Wataalamu wa afya walitumia lectin inayozalishwa na bamia kwa ajili ya kutibu seli za saratani ya matiti (breast cancer). matokeo ya utafiti huu ulionesha kuwa seli za saratani zilipunguwa kwa asilimia 63 na zilikufa kwa asilimia 73. tafiti nyingi zinahitajika kufanywa kuhusu swala hili.
Pia ndani ya bamia kuna folate. Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa watu ambao hawapati kula fotate za kutosha wapo hatarini zaidi ya kupata saratani ya matiti, nyia ya uzazi, ini na aina zingine za saratani. Pia baadhi ya tafiti zilizofanya mwaka 2016 zainaonesha kuwa fotate inaweza kuzuia athari za saratani ya matiti.
Tafiti pia zinaonesha kuwa folate ambayo hupatikana kwenye bamia husaidia katika kuzuia matatizo wakati wa ujauzito. Tafiti zinaonesha mwanamke ambaye hana folate za kutosha anakuwa hatarini kupoteza ujauzito wake au mtoto akajapata matatizo ya kiafya baadaye. Fotate ni muhimu sana kwa mwanamke wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha.
Mwaka 2011 tafiti za kisayansi zilikuwa zikichunguza athari ya bamia kwa wenye kisukari. Wataalamu walitengeneza poda kutokana na maganda ya bamia na mbegu zake. Kisha wakatumia katika kutibu kisukari kwa panya kama majaribio. Panya huyu alikuwa na tatizo la sukari ya kushuka. Matokeo haya yakaleta athari chanya. Hivyo inashauriwa kwa wenye kisukari kutumia sana bamia.
Tafiti zilizofanya na AHA (American Heart Association) zimesema kuwa kula chakula chenye kambakamba (fiber) hupunguza athari hasi za cholesterol ndani ya damu. Vyakula hivi pia hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke (kupalalaizi).
Tafiti zinaonesha kuwa vyakula vyenye vitamin K kwa wingi kama bania ni mujarabu sana katika kuimarisha afya ya mifupa. Vitamin hivi husaidia mifupa kufyonza madini ya calcium. Watu wenyekula vitamin K kwa wingi wana mifupa imara na isiyokuwa na mipasuko (hii ni nadharia tu).
Bamia husaidia katika kuzuia kupata tatizo la kukosa choo kwani kuna kambakamba ndani ya bamia, hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula na kusafiri kwa chakula kutoka tumboni kuelekea maeneo mengine kwenye almentary canal. Bamia hupunguza hamu ya kula, hivyo husaidia katika kupunguza uzito.
Pia itambulike kuwa zipo athari hasi za kula bamia kwa kupitiliza. Kwa mfano bamia hupunguza hamu ya kula, pia bamia huweza kupelekea kujaa gesi tumboni na kujaza tumbo. Kula bamia nyingi zaidi huweza kupelekea kupata vijiwe ndani ya figo kwani bamia zina madini ya calcium kwa wing
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu upungufu wa vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula zaituni
Soma Zaidi...Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.
Soma Zaidi...