Sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.

Post hii inahusu zaidi sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, kuna wakati mtoto anapozaliwa anaweza kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kwa sababu zifuatazo.

Sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.

1. Sababu ya kwanza ni pale mtoto anaposhindwa kuzunguka na kuruhusu bega lipite.

Kwa kawaida ili mtoto aweze kuzaliwa kabla ya kumvuta kutoka kwa mama ni lazima kubadilisha upande au kuzungusha upande ili kuruhusu bega kupita ila kuna watoto wengine hawafanyi hivyo kutokana na sababu mbalimbali hali inayosababisha watoa huduma kuvuta mtoto kwa nguvu wakiwa na lengo la kuokoa maisha ya Mtoto na hatimaye baadhi ya nevu kuachia na kusababisha mtoto  kuvunjika hasa hasa kwenye bega na shingo kwa hiyo utaona shingo la mtoto linacheza cheza na mkono hauna nguvu.

 

2. Pengine kinachosababisha mtoto kuvunjika ni mtoto juwa na uzito mkubwa.

Kwa kawaida uzito wa mtoto ni kuanzia kilo mbili na nusu mpaka tatu na nusu ila kuna watoto wengine unakuta wana uzito kuanzia nne mpaka tano kwa hiyo kuja kutoka nje wakati wa kuzaliwa ni shida nguvu za ziada zinapaswa kutumika ili kuweza kumvuta mtoto ili atoke nje katika kupambana na hali hii usababisha mtoto kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kama vile mkono, shingo na kupata maumivu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

 

3. Mtoto kutanguliza matako 

Hali hiyo pia usababisha mtoto kuvunjika kwa sababu kuja kumzalisha mtoto wa hivi kwa sababu pengine anakiwa ametanguliza matako na mguu mwingine unakuwa umejikunja kwa hiyo kuja kuutoa unakuta umevunjika.

 

4. Mtoto kukaa vibaya.

Unaweza kukuta mtoto katanguliza mkono mmoja mwingine umejikunja hali ambayo usababisha kuvunjika kwa mkono uliojikunja kwa sababu hujui umejikunjia wapi.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/11/14/Monday - 10:24:30 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1010


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-