MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)
Kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wa mwanamke katika mzunguruko wa siku zake. Cervical mucus ni majimaji yenye sifa tofauti tofauti yanayopatikana kwenye njia ya uzazi yaani uke. Majimaji haya yanabadilika kulingana na siku ama maradhi. Miongoni mwa sifa hizi ni kama kinata, kuteleza, kufutika, ukavu na rangi yake.
Majimaji haya yanasaidia katika kutujulisha siku ambazo ni mujarabu kwa wale ambao wanatafuta ujauzito. Pia majimaji haya ni taarifa kuwa yai lipo karibu ktolewa hivyo ni vyema kujiandaa. Majimaji haya pia yanaweza kutujulisha kama mimba imeingia ama laa. Tofauti na kazi hizi majimaji haya yana kazi zifuatazo:-
1.Kuzuia bakteria na wadudu wengine wasiingie ndani kwenye tumbo la uzazi
2.Kusafirisha mbegu za kiume (sperm) kuelekea ndani
3.Kulainisha njia ya uke na kuwa katika hali iliyo bora zaidi.
Majimaji haya huweza kutofautiana muonekano kutokana na mabadiliko ya siku. Siku hizi huanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa hedhi. Ili kuchunguza majimaji haya inahitaji muda na ni vyema kutokukutana kimwili kama unataka kuchunguza mabadiliko haya katika mwezi wote hii husaidia kwani kukutana kimwili kunaweza kuathiri muonekano wa majimaji haya.
Kama unataka kuchunguza kwa baadhi ya siku tu kama kutaka kujua kama yai linakaribia basi unaweza kukaa mkao wowote ambao utafanya uke uwe wazi, kisha tumia kitambaa laini cheupe na kiingize ndani na fanya kama unapangisa kitu kwa ndani ili kuweza kuyapata majimaji haya kwa wingi. Ia unaweza kutumia kidole, baada ya hapo chunguza vyema rangi na muinekano wa majimaji haya kama kuteleza, kunata, kuvutika na uzito.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali za kutokwa na damu baada ya hedhi hili ni tatizo ambalo uwapata wanawake wengi pamoja na akina Mama kwa sababu ya kutokwa na damu yenye utelezi baada ya hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali yanayodhoofisha afya za wanaume, kwa wakati mwingine wanaume ukosa kujiamini kwa sababu ya mambo ambayo yanaadhiri afya za wanaume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kujiepusha na maradhi ya ini
Soma Zaidi...Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.ni mwingiliano unaokuwepo ambao usababisha Mama kukojoa sana wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi.
Soma Zaidi...