Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
DALIILI YA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14)1.Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo joto la mwili wako lilikuwa kubwa, kama ulishiriki tendo siku moja ama mbili kabla ama siku ile, basi endapo joto la mwili litakuwa endelevu hii huashiria huwenda ulibeba ujauzito. Kwa nini, ni kwa sababu joto la mwili hutokea baada ya mabadiliko ndani ya mwili hususani homoni mpya huzaliwa kwa ajili ya kuandaa ukuaji wa ujauzito. Mabadiliko haya ya joto yasifananishwe na joto la homa.
2.Katika wiki hii ya kwanza unaweza kuona mabadiliko ya majimaji kwenye uke. Majimaji yaliyokuwa siku za nyuma kidongo yanaweza kuanza kuchukuwa sura ya mfanano wa majimaji meupe ya yai lililovunjwa. Halikadhalika matarajio ni kuwa uke unatakiwa urudi katika hali ya ukavu baada ya kupita siku hatari. Lakini kama ujauzito ulitungwa uke hautarudi katika hali yake ya kawaida ya ukavu hivyo huanza kuzalisha majimaji kwa wingi. Mabadiliko haya si rahisi kuyaona ila endapo utakuwa manini zaidi unaweza kugundua.
3.Kutokwa na damu kidogo (implantation bleeding). damu hii inaweza kutokea mwishoni mwa wiki ya kwanza ama katikati ya wiki ya pili. Damu hii ni kidogo na inaweza kuwa ni matone kadhaa. Haifanani na damu ya hedhi na wala haitoki na maumivu. Damu hii si endelevu inaweza kutoka kwa muda mchache na kukata. Mwanamke anaweza kuona nguo yake ya ndani inamadoa ya damu. Kwa damu hii mwanamke hatahitai kuvaa pedi.
4.Maumivu ya kichwa ama kichwa kuwa chepesi. Hali hii inaweza kuandamana na kizunguzungu. Hali hii si lazima kuipata, hata hivyo wanawake wengine wanaipata ila hawafikirii kuwa ni tatizo kwani hutokea na kuondoka bila ya kuathiri mwili kwa muda mrefu. Hapa anaweza kuona ni hali ya kawaida kama hatatilia maanani mabadiliko haya.
Kumbuka dalili hizo tajwa hapo juu ni ngumu kuziona mpaka uwe makini sana kwani zinaweza kuathiriwa na hali nyingine za kiafya. Kwa mfano joto la mwili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama maradhi, uchovu na stress. Majimaji ya ukeni yanaweza kuongezeka kwa sababu ya njia za uzazi wa mpango ama mabadiliko ya homoni.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazosababisha kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v
Soma Zaidi...Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.
Soma Zaidi...Kipimo cha Mlimba huweza kuonyesha mimba changa mapema sana. Pia ni rahisi kutumia na kinapatikana kwa bei nafuu. Je ungeoendavkujuwa ni muda gani kinatoa majibu sahihi?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho.
Soma Zaidi...