Faida za uzazi wa mpango kwa jamii

Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa jamii, tunapaswa kujua kuwa uzazi wa mpango ukitumiwa vizuri na jamii nayo inapata faida kwa hiyo zifuatazo ni faida za uzazi wa mpango kwa jamii.

Faida za uzazi wa mpango kwa kwa jamii.

1.Kwanza kabisa jamii inapotumia uzazi wa mpango usaidia Watu kupata sehemu ya kuishi kwa sababu Watu wanakuwa wa kawaida na serikali inaweza kuwapatia sehemu ya kuishi Watu wake.

 

2.Pia  tunaweza kupata huduma za kijamii kwa urahisi, kwa kutumia njia za uzazi wa mpango huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi kwa mfano hospitali, shule na mambo yote yanayohitajika kwa sababu serikali inaweza kuwapatia watu wake mahitaji ya msingi.

 

3.Pia kwa kutumia njia za uzazi wa mpango Watu wanaweza kupunguza hali ya kukosa ajira kwa sababu ya Watu kuwa wachache na serikali na taasisi binafsi zina uwezo wa kuweza kuwaajili Watu wake kwa hiyo tunapaswa kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuweza kupunguza tatizo la ajira

 

4.Pia kwa kutumia njia za uzazi wa mpango, jamii inaweza kuwa na furaha na ushirikiano kwa sababu idadi ya Watu kwenye mazingira ni ya kawaida na rahisi kupanga kitu kikatimilika kwa sababu mnajuana nyingi kwa nyinyi kwa hiyo ni vizuri kabisa na Watu wanaishi kwa amani na furaha.

 

5.Kwa hiyo jamii inajua wazi umuhimu wa uzazi wa mpango, inapaswa kuwaiza Watu kutumia njia hizi za uzazi wa mpango ili kuweza kuondoa matatizo yanayotokea kwenye jamii kama vile huduma za kijamii , kukosa ajira, kukosa makazi na mambo mengine kama hayo.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/21/Monday - 03:39:56 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 979


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-