Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi.
4.SURATUL-MASAD
Sura hii pia ni katika sura za kushuka Maka. Wanaeleza Maulamaa kuwa sababu ya kushuka sura hii ni kuwa mtume (s.a.w) alipopewa amri ya kulingania bila ya siri aliwaita watu wa Maka ili awalinganie na hapo baba yake mdogo Mtume (s.a.w) aitwaye Abdul al Uzza ambaye Qurani imemuita Abuu Lahabi yaani baba wa moto alitowa maneno ya upumbavyu na upuuzi juu ya ujumbe wa Allah na hapo Allah akateremksha sura hii.
Huyu Abu Lahab jina lake hasa ni Abdul Uzza, naye alikuwa baba mdogo wa Mtume s.a.w. Neno Abuu Lahab - baba wa miali ya moto - ni jina ambalo hutumika kwa ajili ya mtu ambaye hali yake n nya asili ni ya moto na ya uasi, na pia hutumika kwa ajili ya mtu ambaye anawachochea wengine. Hivyo bwana huyu amepangwa jina hili na Qur'an kwa sababu ya uadui wake kwa Mtume s.a.w.
Siku ya kwanza Mtume alipowaita Wakureishi ili kuwaeleza habari za ujumbe wake, huyu Abu Lahab, alimkaripia akasema, "Uangamizwe, je umetuitia maneno haya!" (Bukhari).
Na ilikuwa desturi yake kila mara kumfuata Mtume aendako na kuwaambia watu wasimsikilize, akisema, Mtume ni jamaa yake na ni mwehu. Kadhalika mkewe Abu Lahab aliyeitwa Ummi Jamil bint Harb, dada wa Abu Sufiyan, alikuwa mwanamke mbaya sana aliyekuwa anamwudhi sana Mtume na kumsumbua na hata kumsingizia-singizia mambo ya upuuzi. Na kwa sababu ya masingizio yake ameitwa mchukuzi wa kuni (Bukhari), ambazo kwazo amejikokea moto wa Jahanamu, (Razi).
FADHILA ZA SURAT HII
fadhila za sura hii ni kama za sura nyingine kuwa utapata thawabu. Hakuna hadithi sahihi iliyonukuliwa kueleza fadhila za surahii kama zinavyotajwa sura nyingine. zipo baadhi ya nukuu zinanukuliwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema "mwenye kusoma sura hii, hatakuwa makazi sawa na Abuu lahab". Haikunukuliwa hadithi hii katika vitabu vikuu va hadith, na sikuweza kupata ushahidi juu ya usahihi wa hadithi hii
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...Has utakwenda kujifunza utofauti was Hadithi Al Quds na Quran
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran
Soma Zaidi...FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
Soma Zaidi...Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran.
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...