Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran.
{بسم الله الرحمان الرحيم}
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥
Sura hii imeteremka Maka kwa makubaliano ya Mufasiruna wote. Pia Jamhuri ya mufasirun wanakubaliana kuwa sura hii ndio ya kwanza kushuka.
Hata hivyo zipo baadhi ya kauli kuwa sura ya kwanza kushuka ni Yaa ayuha al mudathir, hii kauli amesema Jabir Ibn Abdllah. Na imesemwa pia sura ya kwanza ni alhamdu amesema kauli hii Abu Maisarah na pia imesemwa sura ya kwanza ni aya ya 151 ya surat al anam . lakini kauli zote hizi sio sahihi. Iliyo sahihi ni kuwa sura ya jwanza ni surat al 'alaq
أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يَنْهَىٰ
[Surah Al-`Alaq: 9]
Aya hii na zinazofuata zinamzungumzia Abujahal mmoja katika maadui wa Mtume Muhammad wakati bado yupo Makkah.
Abujahal alikuwa akimuudhi Mtume hakuishia hapo pia alikuwa akimzuia kufanya ibada. Sio hivyo tu pia alikuwa akizuia watu wengine wasiende kwa Mtume wala kukutana nae.
Abujahal alikufa kwenye vita vya Badri na aliburutwa kifudifudi kuelekea kwenye shimo la kuzikia. Na wenzie wengine kama Abulahab alikufa siku chache baadaye.
Allah anasema:
9. Umemwona yule anaye mkataza
10 . Mja anapo sali?
11. Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
12. Au anaamrisha uchamngu?
13. Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
14. Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
15. Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
Umeionaje Makala hii.. ?
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii
Soma Zaidi...Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r.
Soma Zaidi...