Je kuna aina ngapi zabusomaji wa Quran
Aina za usomaji wa qurani:
Wataalamu wa elimu ya tajweed wamegawa aina za usomaji katika makundi makuu yafuatayo;-
1.At-Tahqiyq huu ni usomaji wa taratibu kwa kuzingatia hukumu za tajwid na kuzingatia maana. Msomaji atasimama panapotakiwa na atapumzika panapotakiwa. Kila herufi itapewa haki yake kulingana na inavyotamkwa.
2.Al-Hadr huu ni usomaji wa haraka kwa kuzingatia hukumu za tajwid. Hapa msomaji atazingatia hukumu zote na anatakiwa awe makini katika kufanya ghunnah. Hapa msomaji anaweza kuvuta kwa kiwango cha chini mada. Yaani kama mada ina haraka 2 mpaka sita anaweza kuishia kwenye mbili.
3.At-Tadwiyr hapa msomaji atasoma qurani kati ya usomaji wa aina mbili tulizozitaja hapo juu. Na huu ndio uso wa kawaida na wengi wa watu watu wanautumia.
Umeionaje Makala hii.. ?
Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina iβrab ( Ω Ω).
Soma Zaidi...