image

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia

(b)Dai la Kunakili Biblia



Aidha wengine wanasema Muhammad alinakili mafundisho ya biblia na halafu akadai kuwa yanatoka kwa Allah (s.w). Lakini inadaiwa kuwa hakunakili kila kitu bali alichagua sehemu fulani fulani alizoziona nzuri. Ushahidi wanaoutoa ni kuwa zipo sehemu katika Qur-an ambazo zinafanana na zile zilizomo katika Biblia. Hivyo, kwa kuwa ilitangulia Biblia kabla ya Qur-an ni wazi kuwa Qur-an ndiyo iliyochota kutoka katika Biblia. Madai haya ni dhaifu kwa sababu zifuatazo:



(i)Muhammad (s.a.w) alisema na kusisitiza kuwa Qur-an imetoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).



(ii)Muhammad hakujua kusoma wala kuandika.



(iii)Nakala ya kwanza ya Agano la Kale (Old Testament) kufasiriwa kwa lugha ya Kiarabu ilipatikana mwaka 900 A.D.Wakati huo ilikuwa imekwishapita miaka 200 tangu Muhamad kutawafu. Ama Agano Jipya (New Testament) lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1616, miaka elfu baada ya Muhammad (s.a.w) kufariki dunia!



(iv)Qur-an (4:82) imesema kuwa lau kama hii Qur-an ingetoka kwa asiye kuwa Allah ingekuwa na khitilafu nyingi. Hivyo mtu mwenye shaka na aitumie fursa hiyo kutafuta khitilafu katika Qur-an.


(v) Isitoshe, ikiwa kuna tungo mbili au vitabu viwili vimefanana, kufanana huko peke yake si ushahidi wa kutosha kuwa kitabu kimoja kimenakili kutoka katika kitabu cha kwanza kuandikwa. Hii ni kwa sababu yawezekana pia kuwa vitabu vyote viwili vikawa vimetegemea au kunakili kutoka katika kitabu cha tatu ambacho sisi hatukijui. Ilivyo ni kuwa Taurati, Injili na Quran ni vitabu vya Mwenyezi Mungu. Hivyo ni wazi kuwa kama Biblia imenukuu aya halisi za Tourati na Injili lazima aya hizo zitafanana na aya za Qur-an,kwa vile zote zinatokana na Allah(s.w).



Isitoshe utafiti uliofanywa na baadhi ya wanazuoni umeonesha kuwa amri kumi za Mungu zilizomo katika Agano la Kale kwa mfano, zimekuwemo katika vitabu vya Wahindu kabla ya kuja kwa Agano hilo la kale. Je, tuseme biblia ilinakili amri hizo kutoka kwa Wahindu? Si lazima iwe hivyo. Pamoja na kufanana huko katika baadhi ya sehemu bado kimsingi Biblia na Qur-an zimetofautiana kiasi kikubwa.



Tofauti za Kimsingi Kati ya Qur-an na Biblia



(1)Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu 73 kwa mujibu wa madhehebu ya Wakatoliki au vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti. Vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40. Qur-an ni kitabu kimoja kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.



(2)Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu, Mitume na maoni ya wanahistoria. Qur-an ni neno la Allah (s.w) tu peke yake. Hata maneno ya Muhammad (s.a.w) hayamo katika Qur-an.


(3)Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya Mitume. Kumbukumbu la Torati siyo tu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu bali pia historia ya maisha ya nabii Mussa (a.s). Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimuliwa na wanafunzi wake. Qur-an inataja habari za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.



(4)Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu mitume hao. Ndio maana wanazuoni Wakikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika lini. Kwa mfano katika Biblia iliyotolewa na Collins iitwayo: Revised Standad Version ya 1971 uk. 12-17 imeandikwa kuwa Mwandishi wa 1 Samweli hajulikani, pia hajulikani mwandishi wa kitabu cha 2 Samweli, 1 Wafalme, 1 Mambo ya Nyakati, Esta, Ayubu, Yona na Habakuki.Hali kadhalika mpaka leo kuna wasiwasi kama kitabu cha Waebrania kiliandikwa na Paulo au na mtu mwengine.Na Encyclopaedia Britannica inakiri kuwa mpaka hivi hatuna uhakika jinsi au wapi vitabu 4 vya Injili vilizuka. Kinyume chake Qur-an yote iliandikwa wakati wa uhai wa Muhammad (s.a.w) na ikahifadhiwa vifuani na mamia ya watu.



(5)Injili 4 zilizomo katika Agano Jipya siyo Injili zote zilizoandikwa. Zilikuwapo Injili nyingine nyingi. Ilifanyika Sinodi (mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua Injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe. Injili ya Barnabas ilikataliwa.Na katika historia ya Kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binaadamu waliokuja baadaye ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe. Katika Uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur-an ama isiwe.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 666


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Aina saba za Viraa vya usomaji wa Quran
Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya Tajwid, na ni ipi nafasi yake kwenye uislamu
Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid. Soma Zaidi...

Hukumu za waqfu na Ibtida
waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:
(vii)Dai kuwa Muhammad (s. Soma Zaidi...

Hoja juu ya kukubalika hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hukumu za Idh-har na id-gham katika laam al-maarifa
Laam al- maarifa inaweza kusomwa kwa idgham au idh-har pindibitakapokutana na herufi za shamsiya au qamariya. Soma Zaidi...

Sababu za Kushuka Surat Al-Masad (tabat yadaa) na fadhila zake
4. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat at Takaathur
Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi Soma Zaidi...

Quran haikutoka kwa Mtu zezeta wala mwenye upungufu wa akili
Soma Zaidi...

MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...