Sababu za kushuka kwa surat al qariah
Surat Al qariah, ni moja katika sura zilizochuka miaka ya mwanzoni mwa utume.
Wanazuoni wa Tafsiri hawakupata nukuu juu ya sababu iliyopelekea kushuka kwa sura hii.
Sura hii imeteremka Makkah na ni katika sura za mwanzoni kushuka. Katika mpangilio wa Quran ipo katika juzuu ya 30 katikati mwa surat al adiyah na surat at Takaathur.
Surat al qariah ina aya 11, maneno 36 na herufi 158. Mtindo wa mwanzo wa sura hii inafanana na surat al haqqah. Na sura zote zimeanza kuzungumzia kiyama.
Aya ya kwanza hadi ya tani zinazungumzia kuhusu kiama, na kuwa watu watafufuliwa na kutawanyika kama nzige. Na majabali na milima haitokuwepo tena.
Aya ya 6 hadi ya 9 inazungumzia kuhusu matendo, na kuwa matendo yote yatapinwa kwenye mizani. Kipimo cha matendo mema kikiwa kizito zaidi basi mtu ataingia peponi. Na kikiwa cha na tendo mabovu ni kizito zaidi mtu ataingizwa motoni.
Aya ya 10 na 11 zinazungumzia kuhusu huo moto wa hawiyah. Hili ni moja ya tabaka za moto wa jahannam.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 web hosting 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil
SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.
Soma Zaidi...Ni ipi aya ya mwisho kushuka katika Quran?
Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi
Soma Zaidi...quran tahadhari
TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.
Soma Zaidi...